GSENGOtV
Timu ya soka kata ya Ibungilo hii leo wametawazwa kuwa mabingwa wa #AngelineJimboCup2018 iliyokuwa na msisimko wa aina yake baada ya kuinyuka Kirumba kwenye hatua ya mikwaju ya penati 4-2.
.
Hadi Dakika 90 za mchezo zinamalizika timu hizo zinachoshana nguvu ya sare ya bao 1-1
Penye utamu hatua ya mikwaju ya penati ilikuwaje basi twende dimbani....
ZAWADI ZIMETOLEWA KAMA IFUATAVYO:-
1.BINGWA TSHS 2,000,000/= + 100,000/= (KUTOKA KWA RPC) - IBUNGILO 2.NAFASI YA PILI TSHS 1,500,000/= + 100,000/= (KUTOKA KWA RPC) - KIRUMBA
3.NAFASI YA TATU TSHS 1,000,000/= - SHIBULA
4.MCHEZAJI BORA TSHS 100,000/= - KELVIN JOHN (IBU)
5.MFUNGAJI BORA TSHS 100,000/= - SAID SAID (IBU)
6.GOLIKIPA BORA TSHS 100,000/= - HUSSEIN KAZMIR (KRMB)
7.REFAREE BORA TSHS 100,000/= - MUSSA MAGONGO
8.TIMU YENYE NIDHAMU TSHS 200,000/= - NYAMHONGOLO
9.MWANDISHI BORA TSHS TSHS 100,000/= EDMUND RUTTA - BARMEDAZ TV
10.MWANDISHI WA GAZETI TSHS 100,000/= SHEILA KATAKULA - MTANZANIA
11.MTANGAZAJI BORA TSHS 100,000/= MARIDHIA NGEMELA - CITY FM
12. KATA WAHAMASISHAJI BORA TSHS 200,000/= KATA YA MECCO
13.MUHUDHURIAJI BORA TSHS 50,000/= MR. WAMBURA - WEO IBUNGILO
14.MTANGAZAJI BORA MCHEZO WA FAINALI TSHS 50,000/= BEYA MWANAMALLA .
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula pia ndio muasisi na mdhamini mkuu wa mashindano hayo amesema kuwa anashukuru wana Mwanza kwa mwitikio wao waliouonesha tangu mwanzo wa mashindano hayo hadi hii leo tamati.
Mbunge huyo amesisitiza kuwa mashindano ya 'Angeline Jimbo Cup' yamelenga kuibua vipaji vipya vinavyopatikana ndani ya jimbo lake lakini pia kuvikuza vile vya zamani huku akiwahakikishia kuwa mashindano hayo yatafanyika kila mwaka mara baada ya kupatikana Timu shiriki kutoka ngazi ya kata pamoja na kuwaomba viongozi na wananchi wa jimbo hilo kuunga mkono jitihada anazozichukua katika kuhakikisha wilaya ya Ilemela inaendelea kuwa tanuru la kuoka na kuzalisha vipaji vya michezo mbalimbali nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.