Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna. |
WATU sita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kupatikana na Pombe ya moshi (gongo) kiasi cha lita 170 huko kijiji cha Malya Wilayani Kwimba, kitendo ambacho ni kosa kisheria.
Tukio hilo limetokea tarehe 16.09.2018 majira ya saa 14:00hrs, hii ni baada ya kupatikana kwa taarifa toka kwa raia wema kwamba katika kijiji tajwa hapo juu wapo watu wanaojihusisha na utengenezaji pamoja na uuzaji wa pombe ya moshi. Baada ya kupata taarifa hizo Polisi tulifanya msako wa nyumba kwa nyumba katika kijiji hicho na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao sita wakiwa na kiasi hicho cha pombe haramu ya gongo.
Watuhumiwa waliokamatwa ni 1.Joyce Lukas, miaka 37, 2.Regina, miaka 18, 3.Agnes Mwita, miaka 42, 4.Agnes Gervas, miaka 49, 5.Mwanaidi Jaribu, miaka 26 na 6.Gabriel Funda, miaka 78, wote wakazi wa kijiji cha Malya. Polisi tunaendelea na mahojiano na watuhumiwa wote, pindi uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, tunatoa onyo kwa baadhi ya wananchi wanaojihusisha na biashara haramu ya pombe ya moshi (gongo) kuwa waache kwani ni kosa la Jinai na endapo mtu/watu watakamatwa hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. Sambamba na hilo pia tunawaomba wananchi waendelee kutupa ushirikiano kwa kutoa taarifa mapema za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Katika tukio la pili, Kwamba wiki ijayo kuanzia tarehe 24/09/2018 na kuendelea Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza tutafanya operesheni kabambe ya kukamata magari ya watu binafsi na ya biashara yaliyowahi kuandikiwa faini na kupewa wiki moja wawe wamelipa faini zao lakini hawajalipa hadi imefika wiki nne na mengine zaidi ya hapo. Hivyo magari hayo yatakamatwa na kukaa katika vituo vya Polisi hadi pale muhusika atakapolipa faini. Hata hivyo kwa wale waliosahau kama gari yake inadaiwa faini au laa aingie kwenye mtandao wa- tms.tpf.go.tz.
Imetolewa na;
Jonathan Shanna – ACP
Kamanda wa Polisi (M) Mwanza.
17 September, 2018
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.