Kikosi cha Yanga kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mawenzi Market katika mchezo maalum wa kumuaga aliyekuwa beki wake, Nadir Harou 'Cannavaro.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro, bao hilo pekee limewekwa kimiani na mshambuliaji, Heritier Makambo (53') kutoka Congo.
Kocha wa timu hiyo, Mkongomani Mwinyi Zahera aliamua kuwatumia wachezaji wa kikosi cha kwanza ili kuweza kujua uwezo wa kila mchezaji binafsi kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mbali na kumuaga Cannavaro, Zahera aliwachagua Mawenzi Market kucheza nao ili kujua pia nidhamu ya kila mchezaji kuelekea mechi hiyo ya Shirikisho ambapo watacheza na USM Alger Agosti 19 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.