ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 21, 2018

CUF WAPATA PIGO TENA, KIONGOZI MWINGINE ATIMKIA CCM

Chama Cha Wananchi- CUF wilayani Liwale, mkoa wa Lindi kimepata pigo tena baada ya kada wake ambae alikuwa diwani wa kata ya Kibutuka, Mustafa Mtegite kutimkia CCM.

Mtegite alitangaza uamuzi wa kuhama ndani ya CUF akiwa kijijini Kibutuka hapo jana mbele ya viongozi wa wilaya wa Chama Cha Mapinduzi.

Hivi karibuni aliyekuwa mbunge wa jimbo la Liwale,Zuberi Kuchauka alihama kutoka kwenye chama hicho nakutimkia Chama Cha Mapinduzi mbele ya katibu mkuu wa CCM,Dkt Bashiru Ally.

Halmashauri ya Liwale nimiongoni mwa halmashauri zinazoongozwa na CUF kwenye mabaraza yake ya madiwani.Halmashauri nyingine ni Kilwa.Ambayo majimbo yake ya Kilwa Kusini na kaskazini yanawakilishwa na wabunge wanaotokana na chama hicho.Jimbo la Kilwa Kusin,Seleman Bungara(Bwege),na Kilwa kasikazini,Veda Ngombale.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.