Suzan Lyimo alitaka kujua kama serikali ina taarifa hiyo na kama inayo wanachukua hatua gani ili waweze kuwasaidia wafanyiwe matibabu ya haraka.
Akihoji swali hilo, Lyimo leo Juni 5, 2018, Bungeni Mjini Dodoma amesema “Hivi majuzi tu kule Kyaka kuna watoto wamezaliwa wameungana nilikuwa nataka kujua kama serikali ina taarifa hii na kama inayo wanachukua hatua gani ili waweze kuwasaidia wafanyiwe matibabu ya haraka ili isije ikatokea kama ndugu zetu marehemu Consolata na Maria.”
Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu “Ni kweli serikali kupitia Wizara ya Afya inayo taarifa ya kuzaliwa kwa watoto mapacha ambao wameungana na tayari tumeshatoa maelekezo kwa mganga mkuu wa serikali ili kuwasiliana na Mganga Mkuu wa Kagera ili kuhakikisha watoto wale wanafikishwa Muhimbili haraka iwezekanavyo ili tuweze kuwatenganisha kadri madaktari watakavyo shauri.”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.