Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kukataa matumizi ya plastiki zinazotumika mara moja na kutupwa.
Katika ujumbe wake kwa munasaba wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani Katibu Mkuu Antonio Guterres amesisitiza umuhimu wa ulinzi na uhifadhi wa baharà na mito dhidi ya matumizi ya plastiki na hivyo kulinda sayari na viumbe vyote vinavyoishi ndani yake.
Amesema ,“Sayari yenye afya ni muhimu kwa mustakhabali wenye mafanikio na amani. Sisi sote tuna jukumu la kutekeleza katika kulinda makazi haya tuliyo nayo.”
Guterres ameongeza kuwa, kila mwaka zaidi ya tani milioni 8 za plastiki huishia kutupwa baharini. Amebaini kuwa chembechembe za plastiki baharini hivi sasa zinazidi idadi ya nyota katika anga huku akisema kuwa kuanzia visiwa vya mbali hadi Arctic, hakuna mahali ambapo hapajaguswa na uchafuzi huo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuwa ifikapo mwaka 2050 bahari zote zitakuwa na plastiki nyingi zaidi kuliko samaki endapo hakutakuwepo na jitihada za kupunguza matumizi ya plastiki.
Katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaotokana na utumizi wa plastiki, nchi kadhaa za Afrika zimepiga marufuku utumizi wa bidhaa za plastiki. Hivi karibuni Kenya ilijiunga na nchi zingine 40 ambazo zimepiga mirufuku plastiki zikiwemo China, Ufaransa, Rwanda, Tanzania na Italia.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.