ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 22, 2018

CCM TARIME WATOA KAULI NZITO BAADA YA KIKAO CHA KAMATI YA SIASA.Na. Clonel Tarime
Uongozi wa CCM Wilayani Tarime umemtaka mkuu wa Wilaya hiyo Glorious Luoga kuwapisha katika Wilaya hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kushindwa kutatua matatizo ya wananchi wanyonge jambo ambalo limesababisha baadhi ya wazee kuhangaika ikiwemo kupingwa na kunyanyaswa kikatiri na kunyanganywa maeneo yao bila kujua wapi pakwenda

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Tarime Mkoani Mara Marwa Daudi Ngicho akiongea na Vyombo vya habari ofisini kwake hii leobaada ya kikao cha Kamati ya Siasa nakutoa Maamuzi ya Pamoja nakusema kuwa wameamua kutoa kauli hiyo ya kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kumuondoa mkuu huyo  wa Wilaya hiyo jambo litapelekea maendeleo na haki sawa kwa wananchi wanyonge

Kauli hiyo imetolewa baada ya uongozi wa CCM  Wilaya kumuita kwa ajili ya mazungumzo kuona  jinsi ya kuwasaidia wananchi na kupata suluhu ya migogoro mbalimbali  iliyopo katika Wilaya hiyo na kutohudhuria kikao hicho huku wakimtuhumu kukwamisha ushindi wa CCM ujao pindi akiendelea kusalia katika Wilaya hiyo kutokana  na kuonekana anaunga mkono  CHADEMA.


'Anasema CCM hawana siri bora CHADEMA wana siri sasa  mtu  huyo  hatufai kama wana ccm na akiendelea kukaa katika Wilaya yetu hakika  ccm haiwezi kushinda uchaguzi ujao wa ngazi mbalimbali ,alisema  Ngicho

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.