Mgeni Rasmi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Baba Askofu Jude Thadeus Ruwaich akizungumza kwenye Mahafali hayo.
"Mwaka 2014 Tanzania ilipitisha rasmi Sera ya Elimu na Mafunzo. Sera hiyo ni maboresho na mwendelezo wa Sera ya awali ya mwaka 1995.
Lengo kuu la Sera hii mpya ni kuwa na watanzania walioelimika na wenye maarifa na ujuzi kuweza kuchangia kwa haraka zaidi katika maendeleo ya taifa na kuhimili ushindani kutoka Kanda ya Afrika Mashariki na kwingineko.
Sera ya elimu ya mwaka 2014 inatambua na kuhimiza umuhimu na ushirikishwaji wa sekta binafsina taasisi za kijamii katika kuchangia elimu nchini hasa ikizingatiwa kuwa kanisa limekuwa kwa muda mrefu ni mdau katika harakati za kutoa elimu na huduma nyingine za jamii."
Ni Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino kilichopo Malimbe Jijini Mwanza ambapo maelfu ya wahitimu wametunukiwa Astashahada, Stashahada na Shahada mbalimbali kw mwaka huu wa 2017.
Sehemu ya wahitimu Shahada ya Kwanza ya Sanaa na Elimu Chuo cha SAUT jijini Mwanza.
Makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT, Dr.Thadeus Mkamwa akizungumza kwenye Mahafali hayo.
"Moja kati ya changamoto kuwa inayowakabili wanafunzi wengi ni pamoja na uwezo mdogo wa Serikali katika kugharamikia ufadhili wa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Napenda kusema kuwa - Sera ya Elimu imetambua changamoto hizi na imetamka wazi juu ya umuhimu wa wadau, wahisani na sekta binafsi kushiriki katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na ushiriki endelevu katika kugharamia upatikanaji wa Elimu ya Juu."
"Nawapongeza wazazi na walei kwa kutambua umuhimu wa Elimu ya Juu kwa watoto wenu. Hakika mmefanya uamuzi sahihi hasa katika kipindi hiki kigumu cha uchumi"
Wahitimu mbalimbali Chuo cha SAUT Mwanza.
PHD
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya Shahada ya Uzamili.
Wahitimu mbalimbali Chuo cha SAUT Mwanza.
Wahitimu mbalimbali Chuo cha SAUT Mwanza.
Wahitimu mbalimbali Chuo cha SAUT Mwanza.
Mhitimu Tupokigwe Ambwene anamshukuru Mungu kwa kunyakua Masters nasi Gsengo Blog twaungana naye kumpongeza. Hongera sana.
Mahafali ya 19 Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza yalifanyika Ijumaa na hizi ni picha za siku ya pili yake naizungumzia Jumamosi (Didemba 09 2017) katika viwanja vya Raila Odinga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.