JIJI la Mwanza limeingia kwenye historia hii leo tarehe 12 December 2017, baada ya kuwa kwenye orodha ya maeneo yanayo tumia ndege zisizo kuwa na rubani katika utoaji huduma za usafirishaji vifaa tiba.
KUTOKA Malaika Beach Resort jijini Mwanza, uzinduzi wa maonyesho ya Ndege zisizo na rubani yaani Drone kubwa zenye uwezo wa kusafirisha angani mzigo wenye kilo 20 hadi 40 umefanyika, naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akizungumza na kusanyiko la uzinduzi.
Ni Ndege ambazo zitakwenda kuhudumia sehemu ya Kanda ya Ziwa tukianza na kisiwa cha Ukerewe, ambacho kimekuwa na changamoto nyingi kufikiwa kwa urahisi, huduma zote za haraka kwa vifaa vya tiba kupitia Bohari ya dawa MSD ikiwa ni pamoja na damu, vitendea kazi vidogo vilivyo muhimu mahospitalini.
Picha ya pamoja wakuu na wadau.
Pichani Kamati ya ulinzi na usalama.
Kutoka COSTECH ni Mhandisi George Mulamala.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Madawa nchini (MSD) Laurean Rugambwa.
Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt. Leonard Subi.
Meza kuu.
Drone kwaajili ya kazi.
Gsengo.
Picha ya pamoja na wakuu wa wilaya.
Picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama.
Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella pamoja na waandishi wa habari.
Ndege hizi zimejikita zaidi katika kushukuma mbele shughuli za huduma za afya yaani usafirishaji, hivyo baadhi hususani ule wa dharula utafanywa na Ndege hizi zilizozinduliwa jijini hapa. . Ni Jambo la kipekee sana ambalo kwa mara ya kwanza nchini linaanzia Mwanza kati ya nchi tatu barani Afrika. Benki ya dunia, Shirika la kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), John Snow, Inc na wabia wengine ndiyo wamesaidia kufadhili matumizi ya ndege zisizokuwa na rubani kusafirisha damu na vifaa vingine vya hospitali kwenye vituo vya afya nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe ambaye mradi huo kwa mara ya kwanza nchi umeelekezwa wilayani kwake Frank Bahati, akizungumza na waandishi wa habari.
Lengo ni kupunguza kwa kiasi kikubwa muda unaotumiwa kutuma akiba ya damu kwenye kliniki za afya katika mataifa ya Afrika kwa njia ya barabara na njia nyinginezo. Mfumo utakaotumiwa utahusisha matumizi ya kamba ama uzio kuunganisha sehemu moja hadi nyingine, na mabonde hadi mabonde yenye makazi ya watu , mfumo sawa na ule umbao ulianza tayari kutumiwa nchini Rwanda mwezi October. Faida ya mfumo huo ni kwamba ndege inaweza kukabiliana na hali ya hewa ya upepo mkali kwa muda . Tanzania, Rwanda na Malawi - ambazo zinatumia aina tofauti za ndege hizi zisizokuwa na rubani kwa usambazaji wa huduma za matibabu - zote zina sheria tofauti kuhusu utumiaji wa ndege zisizokuwa na rubani , suala ambalo lilizifanya kuwa mahala pema kwa majaribio ya aina hii
Arusha Yasimama Kwenye Maombi: Miaka 63 ya Uhuru
-
Viongozi wa dini ,mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda na wananchi
wakiendelea na maombi katika matembezi ya kuombea mkoa wa Arusha na
maathimisho ya mi...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.