ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 1, 2017

PICHA ZA RAIS MAGUFULI UZINDUZI WA KIWANDA CHA KUZALISHA BIDHAA ZA PLASTIKI MWANZA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akikagua moja ya mifuniko ya ndoo inayozalishwa na kiwanda cha kutengeneza bidhaa za plastiki na mifuko ya vifungashio Victoria Moulders Ltd na Victoria Polybags Ltd jijini Mwanza hii ikiwa ni mara baada ya kuzindua kiwanda hicho, pembeni yake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Harjeet Singh Mangat.
 Rais Magufuli pia alijionea uzalishaji unaoendelea kiwandani hapo ikiwa ni pamoja na mabomba ya maji na viwanda, ndoo, matanki ya maji, mabomba ya kupitishia nyaya za umeme, viti vya plastiki, mabeseni, madyaba, mabomba mbalimbali kwaajili ya visima na shughuli za migodini.
 Miradi hii ya viwanda ilianzishwa kwa lengo la kupanua Sekta ya Viwanda Nchini na kukuza ajira  katika jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa yenye uhitaji mkubwa kutokana na fursa ya kuwa na shughuli za Kilimo, Uvuvi na Migodi.
 Ziarandani ya kiwanda.
Mhe. Rais akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa kiwanda hicho Harjeet Singh Mangat.
 Uzalishaji ukiendelea.
 Kutoka jengo moja la uzalishaji hadi jingine, Rais JPM mguu kwa mguu na msafara wake.
 Hapa ndipo uzalishaji wa viti vya plastiki huzalishwa.
  Akiwa ameambatana na mkewe (Mama Janet Magufuli) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akikagua moja ya vitengo vya uzalishaji viti vya plastiki vinavyozalishwa na kiwanda cha kutengeneza bidhaa za plastiki na mifuko ya vifungashio Victoria Moulders Ltd na Victoria Polybags Ltd jijini Mwanza hii ikiwa ni mara baada ya kuzindua kiwanda hicho, pembeni yake ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho Harjeet Singh Mangat naye mwenyeji wa ugeni huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela.
 Mashine za uzalishaji.
 Safari ya kutembelea kiwanda na kukagua ikiendelea.
 Malighafi kwenye mitambo.......
 Uzalishaji ukiendelea nayo ziara inaendelea hapa.
 Kiwanda hiki pia kinatengeneza na kuzalisha mifuko yaani PP Bags kwa matumizi ya kuhifadhia vyakula, madawa, mbolea na pembejeo, pia mbegu za mazao mbalimbali.
 Salaam kwa wananchi na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda waliohudhuria uzinduzi huo.
 Salaam kwa viongozi mstari wa mbele.
 Wafanyakazi zaidi ya 500 wameajiriwa na kiwanda hiki.
"Kazi yangu ni kuvikuza na kuvilinda viwanda vya ndani"
 
"Ninazo taarifa za kiwanda hiki jinsi kinavyochangia pato la taifa kutokana na kodi ambazo hutozwa na TRA"

"Kiwanda hiki kimekuwa mstari wa mbele katika kutoa mchango kwa vijana na wananchi wa jinsia zote katika mkoa wa Mwanza kwa kuchangia kukidhi tatizo la ajira kwa taifa"

"Kiwanda hiki kimeweza kutatua na kupunguza uhaba na usumbufu wa upatikanaji wa bidhaa mbalimbali za plastiki ambazo zilikuwa zikiagizwa toka nje, nchi kama China na Kenya hivyo kuondoa hali iliyokuwepo ya kuwa tegemezi wa bidhaa"

Ni moja kati ya kauli za Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage
"Watu wanaosema kwamba kuna matatizo Tanzania, huo ni upotofu, Waje wajionee, Waje wawekeze, sisi wafanyabiashara ni mashahidi kwamba Serikali ipo tayari, TIC wapo tayari kwaajili ya kuwezesha wawekezaji, kikubwa cha msingi ni kuziheshimu tu sheria, miongozo na taratibu zilizowekwa" asema Aritaf Mansour.
Serikali ya Viwanda inawezekana.
PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA/ GSENGO BLOG

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment