ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, October 31, 2017

MAGUFULI AWATOA HOFU WAWEKEZAJI SEKTA YA VIWANDA NCHINI KUHUSU SUALA LA KUKATIKA KWA UMEME


Rais wa Tanzania Dr John Magufuli amewataka wawekezaji nchini na nje ya nchi kuondoa shaka juu ya changamoto ya kukatika kwa umeme iliyojitokeza siku za hivi karibuni hata kutishia baadhi yao kuhisi kwamba taifa linaelekea kwenye mgao.

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba 31, 2017 mara baada ya kufanya ziara yake na kisha kuzindua rasmi kiwanda cha Victoria Moulders Ltd cha jijini Mwanza.

Magufuli amesema kuwa changamoto hiyo ilijitokeza kutokana na ongezeko la matumizi makubwa kiasi cha Megawatt 1460, ambapo tayari Serikali yake inalisimamia hilo kwa kuongeza uzalishaji zaidi wa umeme na hivi karibuni Kinyerezi 1 and 2 zinatazamiwa kuongeza Megawatt 565 zitakazoingizwa kwenye Gredi kuu ya Taifa, vilevile Kinyerezi 3 and 4 nazo zitakuwa na nyongeza ya Mega watt 600 hivyo kuelekea kwenye utatuzi madhubuti unaoiondosha hofu kwa wawekezaji.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment