WAKAZI WA
MJI WA SENGEREMA WILAYANI HUMO WAMEILALAMIKIA MAMLAKA YA MAJI KATIKA
HALMASHAURI HIYO KWA KUKOSA MAJI NA KUPELEKEA KUTUMIA MAJI YA LAMBO AMBAYO
YANAWEZA KUPELEKEA KUHATARISHA AFYA KWA WAKAZI HAO
Wakizungumza na Jembe Fm wakazi hao
wamesema ni zaidi ya wiki mbili sasa wanatumia maji ya lambo ambayo si safi na
salama kwa matumizi ya binadamu kwakuwa yamekuwa yakitumiwa kunyweshea mifugo
mbali mbali,kufulia na hata kuoshea magari
Naye diwani
wa Ibisabageni mh:Jumanne Masunga amesema kuwa maji imekuwa kero kwa wananchi
kutokana na mradi mkuwa wa maji Nyamazugo kuzinduliwa hivi karibuni na mh;Rais
Magufili,na kishahuri mamlaka husika kutanzua kero hiyo kwa wananchi
Akizungumza
kwa njia ya simu meneja wa mamlaka wa maji wilayani sengerema bwana CHRISTOPHAR
KIONE amesema kuwa juhudi za kutanzua tatizo hilo zinaendelea
kuwanyika na kuwataka wananchi kuwa na
subira wakati wowote tatizo hilo litakwisha
Kutokana na
kero hiyo bei ya maji imepanda kutoka
shilingi miambili kwa ndoo hadi shilingi miatano kwa ndoo na maji hayo si safi
na salama
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.