Kim Jong-un ametoa amri hiyo
katika kikao cha maelezo kwa makamanda wa kijeshi wa nchi hiyo kuhusiana
na mpango wa kushambulia kisiwa cha Guam, magharibi mwa bahari ya
Pasifiki.
Katika kikao hicho, Kim Jong-un amesisitiza kuwa, Marekani inatakiwa ifuate chaguo sahihi litakaloweza kuzuia kutokea vita katika eneo la Korea. Aidha kiongozi huyo wa Korea Kaskazini amewataka makamanda wa jeshi kuliweka tayari jeshi la nchi hiyo kufanya mashambulizi tarajiwa ikiwa kutahitajika kufanya hivyo.
Moja ya makombora ya Korea Kaskazini

Tarehe 10 ya mwezi huu serikali ya
Pyongyang ilitangaza habari ya kukamilika mpango wa kushambulia kambi ya
jeshi la anga ya Marekani katika kisiwa cha Guam na kwamba baada ya
kukamilika mpango huo itauwasilisha kwa Kim Jong-un mwenyewe.
Kwa mujibu wa mpango huo, Korea Kaskazini itashambulia kambi hiyo ya kijeshi ya Marekani kwa makombora manne ya balestiki ya masafa ya wastani aina ya 'Hwasong-12' kwa masafa ya kilometa 3200.
Guam ni kisiwa kilichopo magharibi mwa bahari ya Pasifiki kikiwa chini ya udhibiti wa Marekani na kinatumiwa na Washington kama ghala la kuhifadhia silaha zake.
Korea Kaskazini na silaha zake

Mgogoro kati ya Marekani na Korea
Kaskazini ulishtadi baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutoa vitisho
vikali kwamba, ikiwa hali ya vitisho itaendelea kati ya nchi hizo basi
Pyongyang itashuhudia moto wa hasira ambao haujawahi kushuhudiwa na
walimwengu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.