ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 12, 2017

SIKU ZA MMILIKI KIWANDA KILICHOCHAKAA CHA NGOZI MWANZA ZINAHESABIKA:- HILI NDILO TAMKO LA MKUU WA MKOA WA MKOA


Mkuu wa mkoa wa \mwanza John Mongela amempa siku 10 mwekezaji aliyebinafsishwa kiwanda cha Ngozi cha Mwanza Tanaries LTD kukifanya usafi na kuanza mpango wa kufufua kiwanda hicho ndani ya miezi sita ijayo.

Mongela alifika kiwandani hapo akitokea kukagua ujenzi wa barabara ya uwanja wandege ambayo iko kwenye upanuzi kuwa njia mbili.

Kiwanda hicho kilibnafsishwa kwa mwekezaji African Tanaries Ltd.

Ameagiza vifaa vilivyohifadhiwa ndani ya kiwanda hicho kuondolewa ndani ya siku 10.

Amesisitiza kuwa anashangazwa na hali ilivyo sasa kwa kiwanda hicho ambacho kingekuwa moja ya viwanda vyenye kuchangia uchumi wa mkoa sanjari na kufanikisha soko la ajira na fursa mbalimbali kwa wajasiliamali kutelekezwa na kugeuzwa dampo na stoo.

Akiongeza kuwa kiwanda hicho ni moja ya rasilimali zilizoachwa na hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere, na anashangaa kuona pamoja na ukuaji wa teknolojia kwa kizazi cha sasa inakuwaje umuhimu wake usionekane tofauti na zama zake za awali ambapo elimu ilikuwa duni na kilikuwa na manufaa kwa taifa.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.