Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kisiwa cha Migingo katika Ziwa Viktoria ni milki ya Kenya.
Kenyatta
ameyasema hayo Jumatano ya leo katika eneo la Mbita, Kaunti ya Homa Bay
na kuongeza kuwa, hivi sasa kunafanyika shughuli za kuchora mipaka ya
kisiwa hicho.
Rais
Kenyatta ambaye alikuwa ameandamana na Naibu wake, William Ruto ametoa
tamko hilo katika hali ambayo Uganda pia inadai umiliki wa kisiwa hicho
na mgogoro huo bado haujatatuliwa. Akiwa katika eneo hilo ambalo ni
ngome ya kinara wa upinzani Raila Odinga, Rais Kenyatta amesema yeye
kama Rais ana jukumu la kuwahudumia Wakenya wote bila kujali mitazamo
yao ya kisiasa.
Kisiwa
cha Migingo kinatajwa kuwa chenye idadi kubwa ya watu duniani kwa
kuzingatia ukubwa wake ambao ni eneo lisilozidi ukubwa wa uwanja wa
mpira, yaani ekari 0.49. Kisiwa hicho kina nyumba zilizoezekwa kwa
mabati, sababu ya kupewa jina “Iron Clad Island”.
Kisiwa cha Migingo (kulia) na Kisiwa cha Usingo katika Ziwa Viktoria
Kisiwa cha Migingo (kulia) na Kisiwa cha Usingo katika Ziwa Viktoria
Samaki aina ya ‘Ngege’ ndio sababu kuu ya kisiwa cha Migingo kuvuma
mno, na kuna kisiwa kikubwa cha Usingo karibu na Migingo ingawa hakuna
anayethubutu kuishi hapo kwa imani kwamba kina mizimwi.
Mgogoro
wa kisiwa cha Migingo ulianza mwaka 2008 baada ya wanajeshi wa Uganda
kukivamia na kuwatimua Wakenya ingawa kimekuwa kikitambuliwa kuwa ni
miliki ya Kenya.
Makubaliano
ya awali kati ya Kenya na Uganda kuhusu kisiwa hiki yalifanywa 2016, na
kwa sasa maafisa wa usalama kutoka nchi zote mbili wanalinda doria
katika kisiwa hicho.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.