Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umeripoti
kuwa ukuaji wa kiuchumi wa Iran umekuwa na taathira chanya kwa uchumi wa
eneo la Mashariki ya Kati.
IMF Imeripoti leo kuwa utendaji mzuri katika mwaka uliopita wa
2016 katika eneo la Mashariki ya Kati ulikuwa ni matokeao ya kuongezeka
pakubwa ukuaji wa kiuchumi wa Iran kwa zaidi ya asilimia 6.5. Mfuko wa
Fedha wa Kimataifa umeripoti pia kuwa uchumi wa Iran umekuwa kutokana na
kuongezeka kiwango cha uzalishaji wake wa mafuta.Kiwango cha uzalishaji wa mafuta wa Iran kwa utaratibu wa miaka.
IMF aidha imetabiri kwamba ukuaji wa kiuchumi wa Saudi Arabia mwaka
huu utaporomoka hadi sifuri. Benki ya Dunia pia huko nyuma ilitoa ripoti
inayoashiria kukua vyema uchumi wa Iran na kulitaja ongezeko hilo kuwa
zaidi ya asilimia sita.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.