ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 9, 2017

WEMA AACHIWA HURU......., MANJI ARUDISHWA KITUO CHA POLISI AKITAKA KUONDOKA.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemuachia huru Wema Sepetu kwa dhamana yaSh5m katika kesi inayomkabili ya kukutwa na misokoto ya bangi.

Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dwa za kulevya aina ya bangi
Wakili Nassoro Katuga amesema mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa Wema Sepetu mnamo tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio watuhumiwa watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.
Msanii huyo na wenzake wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na wadhamini wawili na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 22 Februari 2017 itakapotajwa tena na kwamba bado uchunguzi unaendelea.

MANJI
WAKATI hayo yakitukia upande wa pili mfanya biashara maarufu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amerudishwa na kushikiliwa ndani ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ambako alifika leo kwaajili ya kuripoti kituoni hapo kama agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda lilivyoainisha jana wakati akitaja majina 65 ya awamu ya pili watajwa wanao tuhumiwa kujihusisha na usambazaji na uuzaji wa madawa ya kulevya..

Manji alirudishwa kituoni hapo akiwa tayari amefika nje akiwa tayari kuondoka.


GWAJIMA
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongozana na wafuasi wake, kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.


Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.