MAMLAKA ya mapato Mkoa wa Mwanza (TRA) imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kwa asilimia 104 kwa kipindi cha mwezi julai 2016 hadi Novemba mwaka jana.
Akizungumza na Gsengo blog jana , Kwa niaba ya Meneja wa TRA Mkoani hapa Ernest Dundee, Ofisa Mwandamizi wa huduma na Elimu ya kodi Lutufyo Mtafya amesema Mamlaka hiyo ilifanikiwa kukusanya Sh Milioni 86.8 kati ya lengo la Sh milioni 83.3 mwaka jana ambayo ni sawa na asilimia 104.2.
Amesema mwaka 2015 kwa kipindi kama hicho lengo lilikuwa Sh milioni 61.1 kati ya makusanyo yaliyopatikana Sh. Milioni 62.5 sawa na asilimia 102.4.
“Mafanikio hayo ya makusanyo ni ongezeko la Sh milioni 24.2 sawa na aslimia 39 kutoka mwaka 2015 hadi Novemba mwaka jana”alisema Mtafya.
Aidha amesema kuwa kwa kipindi cha Julai Mamlaka hiyo imefanikiwa kwa kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa mapato ya serikali kwa kutumia mikakati mbalimbali waliojipangia kwa kushirikiana na Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Lutufyo ameeleza wanatarajia kurasimisha biashara ambazo hazijasajiliwa wakiwemo wachimbaji wa madini na wadau wao kwa ajili ya kuchangia ulipaji wa kodi.
“ Hata hivyo Kushuka kwa upatikaji wa samaki kumepunguza uuzaji wa minofu nje ya nchi na hivyo kupunguza upatikanaji wa kodi za mapato”alisema Mtafya.
Hata hivyo amewaomba wananchi kuendelea kutimiza wajibu wao wa kujisajili kuwalipa kodi kwa wakati na kudai risti sahihi wakati wanapofanya miamala.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.