Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia 'Miss World', ameilalamikia kamati ya mashindano hayo kwa kumtelekeza.
Mrembo huyo ambaye kwa sasa anatakiwa awe kwenye maandalizi ya mashindano ya Miss World, amesema bado hajapata msaada wowote kutoka katika Kamati ya Miss Tanzania na serikali, ikiwa zimebaki siku chache kuweza kufikia kwenye mashindano hayo ya dunia.
Amesema kuwa kwa sasa yeye anachohitaji ni suport pamoja na msaada mkubwa kutoka kwa serikali, kwani yeye binafsi anajitahidi kufanya pale anapoweza.
"Tanzania, viongozi, serikali, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up, kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i deserve", alisema Diana.
Juhudi zinaendelea kuisaka Kamati ya Miss Tanzania kujua nini hatma ya mrembo huyo....
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.