Milango imefunguliwa kwa Wakala wa Usajili na Utoaji wa Leseni za Biashara nchini (BRELA) pamoja na Chama Cha Haki miliki Tanzania (COSOTA) kushiriki katika Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki (MEATF) kutoa elimu ya umuhimu wa kuwa na Hatimiliki na Usajili wa makampuni ili kudhibiti makampuni feki, wezi wa teknolojia na kazi za wabunifu wetu nchini.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda
na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema, ametoa rai hiyo leo Jijini Mwanza,
wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye kusanyiko la utoaji taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza kushika kasi mnamo mwezi Agosti 26 hadi Septemba 4 mwaka huu 2016 katika viwanja vya Rock City Mall.
Lema amesema kuwa wajasiliamali wengi nchini kutokana na kukosa elimu ya umuhimu wa kusajili bidhaa zao, huibiwa ubunifu wao katika utengenezaji wa bidhaa zinazotoka kwenye viwanda vyao vidogo vidogo, ambapo makampuni mengine hutumia mwanya huo kuiba teknolojia, kuiboresha, wakisajili na kuanza kuzalisha bidhaa hizo wakidai ndiyo waanzilishi, hali ambayo huwanyima haki waanzilishi asilia.
"Ipo haja sasa ya kuwaita BRELA na COSOTA, kushiriki maonesho haya, watumie makusanyiko ya wajasiliamali na wafanyabiashara wa viwanda vidogo kuwapa elimu ili wasiibiwe ubunifu wao" alisema Bw. Leopard Lema,
"Maonesho haya yatasaidia kampuni zetu za Afrika mashariki kuweza kupambana na masoko ya hadhi za kimataifa kama vile AGOA, EPA, EBA hivyo tunatengeneza mazingira kwa wafanyabiashara wetu kuingia katika hiyo mikataba na kufanya nayo kazi katika ngazi za kimapinduzi"
Wana-habari kazini. |
Tukipata fursa kubwa Mwanza, na sisi wana Mwanza tutaneemeka zaidi kupitia shughulizetu za huduma na biashara zitakuwa kwa kasi.
This Exhibition aims at achieving the following:-
- To provide an opportunitiy for companies within Tanzania and East African Community to enhance brand and corporate image.
- To provide an opportunity Develop and cultivate customer relation, search for partners and act as market resrarch instrument.
- To tape the opportunity of Mwanza Region as the best available market and Investment area with its excellent strategic location in East Africa.
- To stage this fair as service to the business community as one of the TCCAI'S core objectives.
- To provide an opportunity for Tanzanian Companies to learn and enhance export trade in order to capture available privileged and ready arranged markets worldwide (i.e. AGOA, EPA, EBA etc)
- To give practical support to the East Africans Community integration efforts.
Makampuni mbalimbali na wadau wa sekta binafsi na zile za Serikali tayari yamekwisha thibitisha kushiriki maonesho hayo, zikiwemo idara mbalimbali za Serikali, mifuko ya hifadhi za jamii ambapo kwa ujumla wao ni washiriki zaidi ya 300 toka nchi za Kenya, Uganda, India, China na wenyeji Tanzania.
Maonesho ya mwaka uliopita yalipata takribani wahudhuria wapatao 250,000 toka Kanda ya Ziwa nayo mategemeo kwa mwaka huu ni kupata wahudhuriaji zaidi ya 450,000.
Asilimia kubwa ya Makampuni yote yaliyopo Afrika ya Mashariki kwa msimu wa mwaka 2015-2016 yalihudhuria maonesho yaliyopita ambapo kutokana na manufaa waliyopata msimu uliopita, tayari yameonesha kila dalili ya kutaka kuwemo tena ndani.
Waandishi kazini. |
Bidhaa na huduma zisizoruhusiwa kwenye maonyesho hayo ni pamoja na Silaha za aina zote, Risasi, Mizinga (Bidhaa za kivita), pamoja na huduma za masuala ya kisiasa na kidini kwani ni Biashara na Uwekezaji tu ndiyo umezingatiwa na kamati ya maandalizi |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.