Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiongoza zoezi la kukabidhi vyeti kwa wahitimu kozi ya utengenezaji mipira ya soka katika Chuo cha D.I.T Tawi la Mwanza, |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiongoza zoezi la kukabidhi vyeti kwa wahitimu kozi ya utengenezaji mipira ya soka katika Chuo cha D.I.T Tawi la Mwanza, |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akiongoza zoezi la kukabidhi vyeti kwa wahitimu kozi ya utengenezaji mipira ya soka katika Chuo cha D.I.T Tawi la Mwanza, |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipokea zawadi yake toka kwa mmoja wa wahitimu. |
Rais wa TFF Jamal Malinzi akipokea zawadi yake toka kwa mmoja wa wahitimu. |
WANAFUNZI 14 wamehitimu mafunzo ya kutengeneza mpira wa miguu yaliyotolewa kwa wiki mbili kwenye Chuo cha Taasisi ya Ufundi (D.I.T) tawi la Mwanza.
Akizungumza katika hafla ya kuwapongeza wahitimu hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema anawapongeza wahitimu hao na wakitumia taaluma yao vizuri wataleta mabadiliko makubwa katika soka nchini.
Mongella ameahidi kushawishi wakurungenzi wa halmashauri za mkoani hapa kununua mipira hiyo iliyotengenezwa na wanafunzi hao kutoka chuo hicho ili kusaidia katika kukuza mchezo wa soka.
Mongella amewaomba wanafunzi hao waendelee kutengeneza mipira bora ili kuhakikisha mipira hiyo inatumika katika Ligi Kuu Bara.
Mongella amenunua mipira 40 kwa ajili ya kuzipa timu ya Mbao fc na Toto Africans zinazoshiriki Ligi Kuu, kila timu ikijinyakulia mipira 20. Kaimu Mkurugenzi wa TAN-TRADE, Edwin Rutageruka amekipongeza chuo hicho kwa kukubali mwito wa TanTrade katika kutoa mafunzo hayo.
Rutageruka ameiomba serikali iunge mkono juhudi za kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini. Rutageruka ameliomba pia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lifanye utafiti kujua mahitaji ya mipira nchini na ameahidi kushirikiana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi katika kutafuta soko la mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.
Mkuu wa chuo hicho, tawi la Mwanza, Albert Mmari alisema wataendelea kutoa mafunzo hayo ili kuzidi kupata wataalamu zaidi na amewapongeza wahitimu wa mafunzo hayo ambao ni Abdallah Juma, Frank Nickson, Zacharia Gervas na Moukthtar Ahmed.
Wengine waliohitimu mafunzo hayo ni Nestory Mkumbi, Seleman Seleman, Asimwe Mganyizi, Magesa Nyakwarya, Mary Massala, Loyce Manyenye na Praxeda Lazary, Kulwa Paul, Benedicto Thomas, Malando Emmanuel, Rashid Kitambi, Clement Mange na Mouktar Ally.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.