Na Peter Fabian.
MAKAMPUNI 300 kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yamethibitisha kushiriki maonyesho ya 11 ya biashara ya Afrika Mashariki (MEATF) nayotaraji kuanza Agosti 26 hadi Septemba 4 mwaka huu katika Jengo la la Bishara la Kimataifa la Rock City Mall jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa Habari jana Makamu Mwenyekiti wa CHEMBA ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo (TCCIA) ya Mkoa wa Mwanza, Leopard Lema (Viwanda), alieleza kwamba maonyesho hayo kwa mwaka huu yatafanyika kwa mara ya kwanza kwenye Jengo la Rock City Mall lililopo jirani na Viwanja vya Furahisha Kata ya Kirumba Wilayani Ilemela.
Lema alisema kwamba maonyesho hayo yenye lengo la kutengeneza mazingira ya kuwakutanisha na wabia, wafanyabiashara na kubadilishana uzoefu pamoja na kukutana na wadau mbalimbali kutoka katika nchi za Jumuiya hiyo, wafanyabiashara kupata huduma na kupambana na masoko ya AGOA, EPA na EBA ili kuwezesha kuuza bidhaa zao.
Makamu Mwenyekiti huyo alisema kwamba wajasiriamali wadogo pia wajiunge kupata uzoefu na kuwawezesha kutangaza bidhaa zao lakini kwa wafanyabiashara wakubwa na wakati kutoka makampuni 300 yaliyothibitisha hadi sasa kushiriki maonyesho hayo ambapo watatumia fursa ya kuzitangaza bidhaa kutoka nchi za Kenya, Uganda, Indiya, China na Tanzania.
“Tunataraji mgeni rasmi katika maonyesho ya mwaka huu atakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye tunaendelea kumwomba, lakini tunatarajia maonyesho ya mwaka huu kutembelewa na watu zaidi ya laki moja (100,000)na kutasaidia wananchi wetu kutoka nchi za Afrika Mashariki kupata fursa ya kuimarisha uhusiano na kudumisha amani na ushirikiano,”alisema.
Naye Katibu wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Hassan Karambi, alisema kwamba maonyesho ya Mwaka huu yatakuwa na kauli isemayo “Kuongeza Biashara na Uwekezaji kwa Nchi za Afrika Mashariki” ambapo mashirika ya utalii ya TANAPA na Ngorongoro yatashiriki kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani na kwenye nchi washiriki wa maonyesho hayo.
“Wafanyabiashara na wajasiriamali wote wanaopenda kushiriki maonyesho hayo wajitokeze na kufika katika ofisi zetu za Chemba Jengo la EXAM Benk kulipia gharama za kujisajili na kujihakikishia uhalali wa kushiriki maonyesho hayo kwenye Jengo la Kisasa la Biashara la Kimataifa la Rock City Mall linalomilikiwa kwa ubiya baina ya Mfuko wa Hifadhi wa ALPF na Halmashauri ya Jiji la Mwanza (MCCCL),”alisema.
Naye Mwekahazina wa TCCIA Mkoa , Majid Igangula (INGANS) alisema kwamba ratiba ya maonyesho hayo itaanza Agosti 26 mwaka huu siku ya Ijumaa, Agosti 27-28 Kamati maalumu ya TCCIA kupitia mabanda mbalimbali ya washiriki kutafuta wafanyabiashara waliopanga vizuri bidhaa zao ili kuweka alama za ushindi, Agosti 30 mwaka huu ni siku ya ufunguzi na Agosti 31 ni kupitia kwenye mabanda.
“Tutakuwa na zawadi za vikombe kwa washindi katika makundi 11 ambayo tutameyatenga na makundi sita ili kuwapata washindi na washindi wa jumla hivyo wafanyabiasha na makampuni yatakayoshiriki wajipange vyema kuhakikisha wanajinyakulia ushindi,”alisema.
Igangula alisema kwamba maonyesho hayo yatakuwa na kingilio mlangoni ambapo watu wakubwa watalazimika kulipia Sh 1000/- na watoto wadogo kulipia Sh 500/- kutakwa na michezo mbalimbali kwa watoto pamoja burudani kutoka kwa wasanii, huku TCCIA ikipiga marufuku ya bidhaa za milipuko, siasa na dini zote.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TCCIA, Tungu Misululu (Biashara), alieleza kwamba wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa watakaofika katika maonyesho hayo wajenge utamaduni wa tabia ya kupenda kununua na kutumia bidhaa za Tanzania ili kuwapa fursa wafanyabiashara kuzalisha zaidi na kuongeza ubora wa bidhaa zao.
“Tukiwa wabunifu na wenye kutengeneza bidhaa bora soko lipo na kubwa tu hivyo wafanyabiashara walitambue hilo lakini wananchi nao watumie bidhaa hizo kwa kuwa na utamaduni wa kununua bidhaa kutoka kwa wajasiriamali wadogo na wafanyabiashara wakubwa na kati ili kuongeza jitihada za Tanzania ya Viwanda lengo likiwa kumuunga mkono Rais Dk John Magufuli,”alisisitiza.
Wito wangu ni wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea maonyesho hayo kujionea bidhaa mbalimbali za Ujenzi, Viwandani, Teknolojia, Mawasiliano (TEKHAMA), usindikwaji bora wa bidhaa za vyakula na vingine vingi ili kureta uhalisia wa kukuwa na kupanuka kwa maonyesho hayo kila mwaka.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.