Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Mwanza John Nzwalile ametangaza kuhama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya chama hicho kutokuwa na demokrasia na kuhamasisha wananchi kutoitii Serikali iliyopo madarakani.
Nwalile ambaye kabla ya kufikia uamuzi wa kuhama CHADEMA alikuwa amesimamishwa uongozi katika chama hicho na amewashauri wananchi kote nchini kuacha kushiriki harakati za kisiasa zenye viashiria vya uvunjifu wa amani katika jamii.
"Kuanzia leo tarehe 30/08/2016 nimeacha nyadhifa zangu zote za CHADEMA, Mimi ni Katibu wa mkoa wa Mwanza, Mjumbe wa Baraza kuu la Taifa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa" Alisema Nzwalile.
NINI KUHUSU UAMUZI HATA KUCHUKUWA HATUA HIYO:-
"Nimechoshwa na siasa za kizushi"
"Nimechoshwa na siasa za kichochezi"
"Siasa za majungu"
Siasa za kuwachonganisha wananchi na Serikali yao"
Nzwalile ameihama CHADEMA wakati huu ikijiandaa na Oparesheni UKUTA ambayo hata hivyo imepigwa marufuku na Serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini.
VIPI MAONI YAKE NA DEMOKRASIA:-
"Hata hivyo demekrasia tunayoidai ndani ya Chama haipo"
"Leo umesikia watu wanasema wana Oparesheni za kupinga udikteta, lakini tujiangalie ndani yetu, Jeh tuna demokrasia ndani yetu?" Alihoji Nzwalile na kuongeza
"Kwamba leo mtu anayebana mafisadi, leo mtu anayekusanya kodi anaitwa dikteta"
"Lakini mimi nilidhani udikteta ni mtu kung'ang'ania madaraka"
Nzalile hii leo amejitambulisha rasmi kuwa shabiki wa CCM akiwataka watanzania kuyapuuza Maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA na badala yake waendelee kumuunga mkono Rais John Magufuli.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.