ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 22, 2016

ASKARI ALIYEUAWA AAGWA LEO JIJINI MWANZA.

Kamanda wa Jeshi a Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu askari John Nyange, katika kambi ya Kigoto jioni ya leo ambapo mwili wa marehemu kesho utasafirishwa kuelekea mjini Moshi kwaajili ya mazishi.
Marehemu John Nyange alizaliwa mwaka 1988 katika hospital ya Mawenzi mjin Moshi, Shule ya msingi alisoma Karanga Primary iliyipo mjin moshi, secondary alisoma Shule ya Kifaru iliopo Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kumaliza elimu ya Secondary marehemu John Nyange alijiunga na jeshi la Polisi mwaka 2010, badae alipata nafasi ya kwenda kusomea cheti cha upelelezi na jinai katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi Kidatu, baada ya kumaliza alipata nafasi ya kwenda kusomea diploma ya IT, na hadi mauti yanamkuta alikua akisomea (degree) shahada ya sayansi ya Habari na mawasiliano katika chuo cha Stefano Moshi Memorial University College....

Marehemu ameacha mke na Mtoto mmoja ! Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesikitishwa na kifo kwa kumpoteza kijana ambaye jeshi bado lilikua linamuhitaji..amesema!!

Alisema itakua furaha kwa jeshi la Polis na kwafamilia ya marehemu itakaposikia wale wote waliohusika katika mauaji Haya wanakamatwa na wanaweza kupatikana na hatia!





Enzi za uhai wake marehemu askari John Nyange, 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
R.I.P

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.