- VETA na Airtel kuongeza kozi 10 VSOMO zisomwe kwa simu
Na mwandishi wetu Arusha
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na VETA imeingia mkoani Arusha kuendelea kutoa uelewa kwa vijana kukamata FURSA na kusomo kozi mbalimbali toka VETA kupitia mfumo wao wa simu ujulikanao kama VSOMO. hadi sasa zaidi ya vijana elfu kumi na nane nchini wamejisajili kusoma kwa mfumo huo wa simu za mkononi huku mikakati yao ikiwa ni kuongeza kozi 10 zaidi ili wanafunzi kuendelea kujisomea.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa mauzo kanda ya kaskazini Bw, Brighton Majwala wakati alipoongea na wajasiliamali na madereva bodaboda waliokusanyika stand kuu Arusha jana,
“Airtel na Mamlaka ya ufundi stadi VETA lengo letu ni kuwafikishia elimu ya ufundi vijana wengi nchini, upande wetu Airtel tunahakiksha mtandao upo vyema ili vijana waweze kusoma bila kukwama, hadi leo hii tayari vijana zaidi ya milioni 18 wameshakamata FURSA hii kwa kupakua aplikesheni au mfumo huu wa VSOMO katika simu zao” alieleza Bw Majwala
Majwala aliendelea kusema kuwa “mpango wetu Airtel na VETA ni kuongeza uelewa kwa vijana ili wasome kozi zilizopo sasa ikiwemo ya ufundi piki piki, umeme wa nyumbani, ufundu simu, ufundi wa aluminium, utaalam wa masuala ya urembo, pamoja na ufundi wa kuchomea vyuma”.
kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel alisema “kutokana na VSOMO kuwa na idadi kubwa ya vijana waliojisajili tayari Airtel kwa kushirikiana na wadau wetu VETA tuko katika utekelezaji wa kuongeza kozi zingine zaidi ya kumi ili kuongeza wigo wa kuchagua pamoja na kuongeza idadi ya wanaosoma na kuhitimu”. alieleza mmbando
“tunampango wa kuongeza kozi zingine 10 kabla ya mwezi wa 12 ambapo sasa hivi tayari VETA wako katika utaratibu wa kuzifanyia kazi kozi hizo ili ziweze kuingia katika mtandao” alisema Mmbando
“Mradi wa VSOMO ni sehemu ya mpango wa Airtel FURSA wenye lengo la kuwawezesha vijana pamoja na kutimiza kauli mbiu ya “Airtel the smartphone network” kwa kujipatia elimu ya ufundi stadi toka VETA kwa smartphone zao” alisisitiza Mmbando
Airtel kwa kushirikiana na VETA nchini ilizindua mfumo wa masomo ya ufundi stadi kwa njia ya mtandao VSOMO mwezi Julai 2016 ambapo mpaka sasa tayari mfumo huu umetambulishwa katika mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Arusha, Morogoro na Mwanza lakini kutokana na uhitaji mkubwa kwa vijana tayari mfumo huo umepokea maombi ya vijana toka mikoa 25 kwa kupakua mfumo/aplikesheni hiyo hiyo na kuomba kusoma kwa njia ya simu za Airtel.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.