Mwanasiasa Moise Katumbi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo anasema kuwa alidungwa sindano iliyokuwa na sumu nje ya mahakama ya Lubumbashi mnamo mwezi Mei.
Katumbi anasema haikujulikana sindano hiyo ilikuwa na nini.
Hata hivyo anasema askari polisi mmoja alimdunga sindano katika mshikemshike nje ya mahakama polisi walipofyatua mabomu ya kutoa machozi kwa mashabiki wake alipokuwa akienda kujibu mashtaka ya kuwaajiri mamluki kuwa walinzi wake kinyume cha sheria.
Bw Katumbi anasema kuwa madai hayo dhidi yake ni ya ''upuuzi''.
Hata hivyo kiongozi huyo ambaye ni mkurugenzi mkuu wa klabu ya TP Mazembe aligonjeka na akalazimika kukimbilia nje ya nchi ilikupata matibabu.
Katumbi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa alikwenda Afrika Kusini Uingereza na kisha Ujerumani kutafuta tiba.
Waziri wa mawasiliano bwana Lambert Mende hakujibu mawasiliano dhidi ya serikali yake lakini kwa siku nyingi amepuuzilia mbali tuhuma kuwa polisi wa DRC walimdhuru bwana Katumbi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.