Dodoma. Wabunge wa Upinzani wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson, huku leo wakitoka bungeni kwa mtindo mpya wa kuziba midomo na karatasi.
Hii ni wiki ya tatu mfululizo wabunge wa Ukawa wamekuwa wakitoka bungeni baada ya kutangaza kuwa hawatahudhuria vikao vyote vinavyoongozwa na Dk Tulia, kufuatia kukataa hoja ya kujadili sakata la kufukuzwa wanafunzi 7,800 wa stashahada maalumu ya sayansi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Wabunge hao wameeleza kuwa hawaridhishwi na uongozi wa wa Naibu Spika na sasa wanaendelea na vikao vyao nje ya Bunge.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi) James Mbatia amesema wameanza kutoka kwa kufunga midomo na karatasi kuambia dunia kuwa bajeti imejaa ghiriba na udanganyifu mwingi kwa Watanzania.
Amesema watakwenda kuwaambia wananchi na hata kama mikutano imezuiwa, Rais John Magufuli asitegemee kwamba watanyamaza.
"Harakati hizi tulizianza tukiwa Chuo Kikuu na Dk Magufuli nilikuwa naye japo alikuwa mbele yangu. Dk Ackson alikuwa shule ya msingi na tangu wakati huo, harakati zinaendelea," amesema Mbatia. ZAIDI BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.