Wakati ambapo dunia inaendelea kuomboleza kifo cha bingwa wa zamani wa masumbwi wa uzito wa juu, Muhammad Ali, rapper wa Bonta anatukumbusha historia kidogo.
Muhammad Ali alikuja Tanzania mwaka 1980 lakini alijikuta akikutana na waziri mkuu peke yake huku Mwalimu Nyerere akigoma kukutana naye. Kwanini?
“Enzi hizo waziri mkuu alikuwa Salim Ahmed Salim na lengo la kufika hapa mashindano ya Olimpiki yalikuwa yanafanyika Russia na yeye akiwa kama Mmarekani alitumwa na ujumbe kutoka Marekani akawa ameuleta Tanzania na kwa bahati mbaya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikataa kuonana naye,” Bonta alimuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Ni kwasababu taifa letu la Tanzania lilikuwa ni Non alignment hatujihusishi na pande yoyote ile Marekani au Russia enzi hizo ikiwa USSR kwasababu kama unakumbuka walikuwa na vita baridi. Sasa Muhammad Ali alikuwa ametuletea ujumbe watanzania kwamba tusiende kushiriki kwenye Olimpiki inayofanyika Russia tugomee mashindano yale,” aliongeza Bonta.
“Kwahiyo aliishia kupokewa na waziri mkuu Salim Ahmed Salim akafikisha ujumbe wake na akarudi kwao Marekani.”
Hata hivyo Bonta anasema wana hip hop wameomboleza zaidi kifo chake kutokana na bondia huyo kuwa mwanaharakati wa haki za watu weusi kitu ambacho muziki wa Hip hop umekuwa ukihusishwa na harakati hizo.
Mazishi ya Muhammad Ali yatanyika Ijumaa hii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.