ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 8, 2016

NYAKATI NYINGINE TUNAPASWA KUWARITHISHA WATOTO KIPAJI CHA UCHAPAKAZI.

KWA kuiga tamaduni za watu wa magharibi bila kujadili kuhusu suala la mazingira, jiografia, uchumi, changamoto za kipato cha mtu mmoja mmoja na mfumo wa elimu yetu isivyo shindani sanjari na mapinduzi ya viwanda kama mataifa mengine, siyo siri tutabaki kulaumu vijana wetu wa leo kukosa ajira, siyo kwa wasio na elimu tu bali hata wale wanaotoka vyuoni kwani hawakuandaliwa kujiajiri na hawana moyo wa kujituma wala hawajui wapi pa kuanzia linapokuja suala la kujiajiri..

Kamera yangu iliwanasa watoto hawa katika soko la jioni la Pasiansi wilayani Ilemela jijini Mwanza. Kwa mujibu wa mazungumzo niliyofanya nao wanasema mara baada ya masomo nyakati za jioni hushiriki zoezi hili la kuwasaidia wazazi wao, zaidi ni mama zao katika shughuli mbalimbali za ujasiliamali wa kusaga karanga za wateja wanaofika sokoni hapo.

Wateja wanapo nunua karanga toka sokoni, karanga hizo hukaangwa na mama wa watoto hawa kisha watoto kushiriki zoezi la kuwasaidia mama zao kusaga karanga hizo kwa kutumia nyenzo hii ya kurahisisha usagaji karanga kama sehemu ya biashara.

Mama ndiye mpokea pesa, ambayo hutumika kwenye kusukuma maisha ya kila siku.
Shughuli hii ni kama kumsaidia mama kuteka maji, kufagia uwanja na shughuli nyingine za nyumbani ambazo humjenga kijana katika makuzi na maadili.
 Mara baada ya mahoojiano nami Gsengo niliwasaidia watoto hawa wenye utii na nidhamu katika kusaga karanga. 

Baada ya kujadili kwa kina nikatoka eneo hilo nikiwa nimejifunza kuwa uchapakazi, kujitegemea na ujasiliamali ni elimu inayokuza toka nyumbani na si mashuleni. Kumbe unaweza kuhitimu madarasa na madarasa, vyuo na vyuo lakini ukashindwa kuendesha maisha ukisubiri uwezeshwaji na uwezeshwaji unaweza ukadunda ukasubiri kumezewa.

Ndiyo maana malalamiko juu ya ajira hayaishi hapa nchini.

Hivi umeshawahi jiuliza kwanini kuna watu wengine ni matajiri ile hali hawajasoma au pengine waliishia madarasa ngazi za chini kabisa? Na kuna wengine wana elimu ya juu lakini wanahaha kutafuta ajira na kuajiriwa?

Jibu ni kwamba familia, jamii na mazingira waliyoishi siku za nyuma ilikuwa darasa tosha kukabiliana na maisha ya mbele.
Eneo la soko la jioni Pasiansi wilayani Ilemela jijini Mwanza.

NYONGEZA>MAGUFULI LAWA NENO JIPYA LA KISWAHILI MAARUFU KENYA
Nchini Kenya mtu akifanya vizuri wanamwita Magufuli. Kwa mfano fundi mzuri wa magari wanamwita Magufuli wa Magari, Mwalimu mzuri wa Hisabati wanamwita Magufuli wa HIsabati. Kwa jinsi lilivyosambaa Kenya laweza ingizwa kwenye kamusi ya kiswahili likimaanisha mtu mahiri katika kitu fulani.
Mfano mzuri soma hapa uone neno Magufuli LILIVYOTUMIKA kwa wenzetu I won't go slow, the 'Magufuli' of Education tells Ndunda - Capital News

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.