*VIJANA JIJINI MOROGORO WACHANGAMIKIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KUPITIA AIRTEL FURSA*
Airtel Fursa imejikita katika mradi wake wa kuwezesha vijana hapa nchini katika ujasiliamali kupitia mpango wake wa kukomboa vijana hapa nchini wa “Airtel Fursa Tunakuwezesha”.
Wito umetolewa kwa vijana hapa nchini kujitokeza katika kuchangamkia fursa za kijasiriamali zinazojitokeza ili kuweza kuwaepushia vijana na matendo maovu yanayoweza kuwafanya ndani ya jamii kukosa thamani.
Rai hiyo imetolewa na Meneja utawala VETA MVTTC Twiganile Ndunguru Mkoani Morogoro katika warsha ya mafunzo ya Airtel fursa kwa vijana wajasiliamali iliyo lenga kuwapatia vijana fursa katika kuendesha biashara zao ili kuweza kujipatia kipato ambapo amesema vijana hao wanatakiwa kijishughulisha na kuachana na mitazamo hasi huku wakipoteza muda mwingi katika michezo isiyoweza kuleta tija katika maisha yao.
Alisema kuwa amefurahishwa sana na mpango huu wa Airtel katika kuwakomboa vijana kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiliamali hapa nchini kwa kuwa anaelewa kuwa vijana wa jiji la Morogoro hususan wasichana wana muitikio mkubwa katika swala zima la ujasiriamali na maendeleo binafsi.
Nae Meneja huduma za jamii Airtel Tanzania Hawa Bayumi amesema Airtel Fursa pia inatoa ujuzi kwa namna gani ya kukabiliana na chagamoto ya mfumo wa biashara ikiwemo leseni za biashara, mtaji wa kufanyia biashara na elimu ya biashara yenye tija ambayo ndio chachu kubwa ya vijana kushindwa kuendelea na biashara zao, huku washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa yamewnufaika kwa kiasi kikubwa kwani wameza kutambua jinsi yakuendesha biashara zao.
Aidha alibainisha kuwa katika mchakato huu wa Airtel Fursa Tunakuwezesha, “Airtel inatarajiwa kuwawezesha vijana wengi hapa nchini kwa kuwapatia vitendea kazi na kuweza kufikisha ndoto zao za kujikomboa kiuchumi na kuweza kujiajiri wao na kuweza kukomboa wenzao. Kwani Airtel inaamini kwamba kwa kumuwezesha kijana hapa nchini, unamuwezesha yeye mwenyewe na jamii inayomzunguka kwa kuleta maendeleo katika jamii hiyo”. Aliongeza Bayumi
Warsha hiyo ilihudhuliwa na vijana zaidi ya 200 ambao wamepewa vyeti vya kushiriki ambapo mafunzo yanawahusisha watu warika mabalimbali kuanzia miaka 18 hadi 24 ambapo vijana hupatiwa mafunzo ya biashara pamoja na kupewa vitendea kazi katika kuendeleza biashara yao ili kuondokana na changamoto wanazo kabiliana nazo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.