Mapema mwanzoni mwa wiki hii magazeti nchini Afrika ya Kusini na baadhi toka nchini Uingereza yamelalama na kutupa madongo ya kejeli kwa mwanamuziki Beyonce, mara baada ya taarifa zilizotoka toka Hollywood zikimweleza mwanamuziki huyo kwamba yuko kwenye hatua za maandalizi ya kutengeneza filamu ya historia ya maisha ya mwanamama Saartjie Baartman, aliyekuwa akitumikishwa kama mtumwa mwenye mvuto ambapo Beyonce ndiye angesimama kama mwanamama huyo.
Kwa kuona hivyo GSENGO BLOG ikaona ni kheri sasa kukupa japo kwa ufupi historia ya mwanamama huyo na hata picha zake ili nawe ufanye mlinganisho na mwisho wa siku upate nafasi ya kukomenti kuhusu hatua hiyo au kama vipi mbelembele ikibidi uwe na pendekezo lako. (ukiamua)Sasa ipate kwa njia ya sauti simulizi ya Mwanamke mrembo "Sarah" Baartman aliyezaliwa miaka ya kabla ya 1790 – 29 December 1815) akifanya kazi kama mtumwa mjini Cap Town nchini Afrika ya Kusini akiwa na sifa ya kuwa na umbo la kiafrika lenye taswira ya kuwa na makalio makubwa ambaye inasadikika kuvunja rekodi kwa wanawake wote waliopata kutokea ulimwenguni hata wazungu wa utawala wa kikoloni kumchukua hadi nchini Uingereza na kumtumia kama maonyesho.
Lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 26 tu...na ni kwa ugonjwa wa zinaa.
BOFYA PLAY KUSIKILIZA Simulizi ya iliyosimuliwa kupitia kipindi cha majira ya jioni kupitia kituo cha radio cha Jembe Fm Mwanza ukiwa na Jaqueline Shuma, Timoth Ngalula na Babu Mkombe.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.