James Lembeli (kushoto) akiwa na Mchungaji Peter Msigwa. |
Oktoba 29,2015.
JEMBE FM KAHAMA.
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama mjini kupitia CHADEMA James Lembeli amekanusha taarifa za yeye kukamatwa na kufikishwa Mahakamani na jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kama ambavyo imevumishwa.
Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari, Lembeli amesema kuwa kuonekana kwake katika eneo la polisi na mahakamani siku ya tarehe 26 mwezi huu alikuwa akishughulikia suala la mawakala wake waliokamatwa na polisi usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi.
Kuhusu afya yake, Lembeli amesema tangu kuanza kwa kampeni hadi leo afya yake ni njema, licha ya kusumbuliwa na sikio mwanzoni mwa kampeni,ambapo tangu siku ya uchaguzi hadi kutangazwa kwa matokeo hajawahi kusafiri kwa ajili ya matibabu.
Katika hatua nyingine amewatoa hofu wananchi wa Kahama juu ya tetesi za kuuzwa kwa Redio yake ya Kahama FM na kusema kuwa sio za kweli,bali zilitengenezwa kwa lengo la kumshushia heshima katika kipindi cha kampeni.
Hata hivyo Lembeli amewaahidi wananchi wa Kahama kuwa ataendelea kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo,kwa kutekeleza ahadi alizoziahidi wakati akiwa mbunge na wakati wa kampeni, ikiwemo ukamilishaji wa ujenzi wa shule za msingi na Zahanati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.