Mgombea ubunge wa jimbo la kibaha mjini kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Silvestry Koka akiwahutubia wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni katika kata za msangani pamoja na kongowe . |
Mwonekana la nyomi la wananchi na pamoja na wanachama wa CCM, wakiwa wanamwaga mgombea huyo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa wa kampeni (Picha zote na Victor Masangu) |
Baadhi ya wazee na wananchi wakiwa wanacheza kwa furaha kabla ya kuazna kwa mkutano huo. |
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
KATIKA kuunga juhudi za serikali katika kupambana na wimbi la umasikini Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amesema kwamba atalivalia njuga suala hilo endapo akichaguliwa na wananchi kwa kuviwezesha kwa hali na mali vikundi mbali mbali vya ujasiliamari vya wakinamama na vijana lengo ikiwa ni kuweza kuleta mabadiliko chanya katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi.
Koka aliyasema hayo wakati alipozungumza na wananchi katika mikutano yake miwlili ya kampeni katika kata ya msangani pamoja na kongowe ambapo alisema kwamba nia yake kubwa ni kuona wananchi wake wote wa jimbo la kibaha mjini wanakuwa na shughuli yoyote ya kufanya ili kuweza kuhakikisha wanaondokana na ile hali ya kuwa tegemezi.
Mgombea huyo alisema kwamba ana imani endapo akiendelea kuviwezesha vikundi vya wakinamama na vijana katika siku zijazo wataweza kujiendeleza wai wenyewe na watapiga hatua kubwa ya kuleta mabadiliko ambayo na wao wenyewe wataweza kupata fursa ya kujiajiri wao wenyewe kutokana na mitaji atakayowapatia.
“Mini ninatambua katika jimbo langu la kibaha mjini nina tambua kuwepo kwa changamoto ya wananachi ambao hawana kazi yoyote ili kwa upande wangu nitahakikisha ninaliwekea mikakati endelevu ya kuhakikisha ninavisaidia vindi vyote vya wakinama na vijana ili waweze kupambana na janga la umasikini na kukuza maendeleo kupitia mitaji amabyo nitawapatia,:alifafanua Koka.
Aidha mgombea huyo alibainisha kwamba katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wakati yupo maadarakani aliweza kufisaidia vikundi mbali mbali vya ujasiriamali amabpo ameshatumia zaidi ya shilingi milioni 480 katika kuwainua wakinamama, vijana pamoja na wazeee hivyo ndoto yake kubwa ni kuendelea kujitoka kwa hali na mali yeye pamoja na familia yakeili kuwakomba wananachi wa kibaha.
“Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita vikundi mbali mbali nimeweza kuvisaidia na nimeshatumia kiasi cha shiningi milioni 450 kwa ajili tu ya vikundi mbali mbali kuviwezesha na kwamba fedha zote ambazo nimwezitoa ni zangu mwenywe na familia yangu hii ni jinsi gani nataka wanaanchi wangu waweze kupiga hatua zaidi ya kukuza uchumi pamoja na kuleta kasi ya maendeleo,”alisema Koka.
Kadhalika aliongeza kuwa mbali na kuziwezesha vikundi kwa vijana na wakinamama amejipanga kuwasaidia vijana kuwapatia ajiara kupitia viwanda mbali mbali ambavyo vimeshajengwa katika Wilaya ya Kibaha mjini ambavyo kupitia fursa zilizopo wataweza kunufainika na viwanda hivyo.
Mgombea huyo katika hatua nyingine aliwahakikishsia wananchi kulisimamia kwa ukaribu suala la changamoto ya uhaba wa madawa katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali kwani limekuwa ni kero kubwa ya siku nyingi kwa wananchi wanapokwenda kupatiwa matibabu huduma ya upatikanaji wa dawa inakuwa ni vigumu kwani wanaandikiwa kwenda kununu sehemu nyingine hali ambayo alisema ni lazima aitafutie ufumbuzi wa kudumu lengo ikiwa ni kuwasaidia wananachi wake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.