NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
KUTOKANA na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa umeme sambamba na kuhujumu miundombinu kwa baadhi ya wanachi na wateja kumelisababishia shirika la ugavi wa umeme Tanesco Mkoa wa Pwani kupata hasara ya zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 40 na kusababisha shirika hilo kupoteza makusanyo ya mapato kama inavyotakiwa.
Hasara hiyo Tanesco imebainika kufuatia operesheni maalumu ya ukaguzi ya mita katika Wilaya ya Kibaha pamoja na Bagamoyo ambapo wameweza kuwabaini wateja wao kufanya uharibifu mkubwa wa mita na hivyo kusababisha kupotea kwa umeme mwingi na kulisababishia shirika kukusaanya mapato kama inavyostahili.
Akizungumzia kuhusiana na zoezi hilo la ukaguzi mwandisi mkuu wa kitengo cha ukaguzi wa mita kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mrisho Sangiwa alisema kuwa kutokana zoezi hilo la ukaguzi wamefanikiwa kuwanasa wezi hao wa umeme wapatao 39 ambao wamehusika katika kuhujumu miundombinu ya shirikika.
Sangiwa alisema kwamba kutokana na tabia ya baahi ya wateja wao kujiunganishia umeme kinyemela kunachangia kwa kiasi kikubwa kupotea kwa umeme ambao wamebaini kuwa unatumika tofauti na matumizi halali ya wateja wao.
“Kwa sasa sisi kama shirika tupo katika zoezi la kufanya ukaguzi wa miundombinu yetu ili kuweza kufahama kami ipo salama au kuna baaadhi ya watu wacheche wameifanyia hujuma kwa kuharibu mita zetu, ila sisi hatuwezi kulivumilia suala hili lazima tupambane na watu kama hawa kwani lengo letu ni kuhakiksha tunatoa huduma iliyo bora kwa wateja wetu,”alisema Sangiwa.
Kwa upande wake Afisa usalama wa Tanesco Mkoa wa Pwani Henry Byarugaba alibanisha kwamba kwa sasa wananchi wanapaswa kuwa makini na kuhakikisha kwamba wanatoa taarifa katika vyombo husika ili kuweza kuwabaini wale wote wanaofanya hivyo ili kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.
“Ndugu mwandishi nadhani na wewe mwenyewe unajionea jinsi miundombinu yetu inavyohujumumiwa lakini kitu kikubwa tumeweza kubaini kuna baadhi ya watu wanafanya ujanja wa kuzichezea mita zetu ili umeme utumike mdogo tofauti na matumizi halali kwa hivyo wateja wa aina hii inabidi tuwawajibishe,”alisema Byarugaba.
Pia baadhi ya wateja ambao hawakutaka kutajwa majina yao walibainisha kuwa ni kweli kuna wananchi wengine wanafanya wizi kwa makusudi hali mbayo wamedai ni hatari sana kwani kunaweza kusababisha kutokea kwa majanga ya moto kutokana na kujiunganishia umememe bila ya kuwashirikisha wafanyakazi wa Tanesco.
Mkaguzi mkuu wa Tanesco kanda ya Dar es Salaam na Pwani Dismas Mbonde alisema kuwa kuna baadhi ya nyumba wamekuta kuna kuna hali ya hatari kwa nyumba zao kupata majanga ya moto kutokana na kujiunganishia nyaya kutoka kwenye nguzo za umeme na kupitisha moja kwa moja bila ya kuingia kwenye mfumo wa mita.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.