NA PETER FABIAN, MISUNGWI.
SHULE msingi ya wanafunzi walemavu ya Mitindo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza, inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji safi na salama, upungufu wa magodoro 175 kwa sasa, vitanda 100, viti vya kukalia 275 na majengo mawili ya mabweni ya wavulana na wasichana.
Akizungumza na MTANZANIA juzi, Mkuu wa shule hiyo, Kurwa Nghwelo, alisema kuwa kukosekana kwa maji limekuwa ni tatizo kubwa la shuleni hapo na kusababisha watoto wenye ulemavu wa ngozi kushindwa kuoga na mavazi yao kufuliwa nguo hali ambayo imekuwa ikiwapa shida kwa watu wanaowasaidia kwa kupoteza muda mwingi kuhangaikia kutafuta maji.
Nghwelo alisema kuwa kutokana na uhaba huo wa maji safi na salama shuleni hapo, walimu wamekuwa wakishindwa kuwafundisha wanafunzi hao wenye ulemavu wa ngozi (Albino) kutokana na miili yao kuwa katika hali mbaya na baadhi kuwashwa kutokana na jacho, huku wengine wakihitaji kuogeshwa ili kupakwa mafuta ya kulainisha ngozi zao kuzuia vipele na muwasho.
Mkuu huyo alisema kuwa changamoto nyingine inayowakabili ni kuwepo upungufu wa vitanda na magodoro zaidi ya 175 ya kulalia hao hali ambayo watoto hao kulala kwenye vitanda vikiwa vimewekewa mabox jambo ambalo hulalamika kuumia mbavu na kuamuka wakiwa wachovu na kushindwa hata kuingia darasani pia kuwepo mbanano kutokana na ufinyu wa mabweni.
“Tunavyo vitanda vingi lakini havina magodoro, shuka za kutandika na kujifunika, hali ni mbaya sana watoto hawa wanahitaji kusaidiwa kutokana na wazazi wao wengine kutofika hata kuwaona tangu wawalete hapa kutokana na hofu ya mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) iliyopo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa na mikoa ya jirani ambapo watoto hawa wanatoka”alisema.
Nghwelo alisema kuwa pia shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa viti vya kukalia wanafunzi wenye ulemavu wakati wakiwa darasani na wakati wa kupata chakula kwenye bwalo jambo ambalo hupelekea watoto wengi kukaa chini na kusababisha nguo zao kuchafuka na kuwafanya wasiwe kwenye mwonekano mzuri wa mavazi yao.
“Wazazi wa watoto wengi waliopo katika hii shule wamewatelekeza watoto wao hivyo wakati wa kufunga shule wamekuwa wakilia wakitaka wazazi wao waje kuwachukua wakasalimie ndugu zao, pia kushindwa kuwaletea mahitaji muhimu ikiwemo mavazi, mafuta, sabuni, shuka na jambo ambalo shule hushindwa kumudu kugharamia watoto wote 202 wenye ulemavu,”alisema.
Aidha alisema kuwa shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 1153 ambapo walemavu wakiwa 202 wakiwa katika makundi matatu ambapo wasioona wakiwa 50, wasiosikia (Viziwi) 71 na wenye ulemavu wa ngozi 81 huku kila mwaka kumekuwa na ongezeko la watoto wenye ulemavu kutoka 20 hadi kufikia 80 jambo ambalo pia ni changamoto kubwa wa kuwalea watoto hao.
Wito wangu kwa Taasisi, Mashirika, Kampuni, Wafanyabiashara na wananchi kujitokeza kusaidia shule hii kwa kusaidiana na serikali ili kupambana na changamoto zinazotukabili ikiwemo na kuongeza majengo mawili ya mabweni, vitanda 150, magodoro zaidi ya 275, viti 300 na kuweka mtandao wa uhakika wa maji safi na salama ili kuwezesha watoto hao kuwa katika mazingira mazuri muda wote.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.