DR. KAMANI: "UTAWALA BORA HAIMAANISHI KUWA LEGELEGE" Rushwa haiwezi kugeuka kuwa mafuta, Rushwa ni Rushwa hivyo lazima ikemewe na idhibitiwe....
Mikakati anayokusudia kuitekeleza katika juhudi za kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania ni kama ifuatavyo:-
1.Kuendeleza na kuimarisha mshikamano wa uongozi unaoshirikisha wananchi katika matumizi ya rasiliali nyingi zilizopo nchini. Rasilimali hizo ni pamoja na bahari, maziwa, wanyamapori, madini, gesi asili, mifugo, ardhi na watu na kujenga umoja wa kitaifa.
2.Kuendeleza kujenga na kuimarisha miundombinu hasa ya barabara, reli na umeme. Miundombinu inayounganisha mikoa ya Tanzania na ile inayounganisha Tanzania na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Msumbiji itatiliwa umuhimu wa pekee.
3.Kuongeza kasi maendeleo vijijini (Rural Development)) ili kupambana na umasikini kwa kuimarisha na kuendeleza umeme vijijini, mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na ufugaji nyuki na uchimbaji madini, matumizi ya teknolojia stahiki, matumizi ya pembejeo na usindikaji mazao na masoko.
4.Kuendelea kuimarisha na kujenga huduma jamii vijijini (afya, elimu, maji miundombinu nk) ili kuimarisha na kuboresha hali za maisha ya wananchi vijijini.
5.Kukuza uchumi kwa kuweka Mazingira bora ya uwekezaji na kufanya biashara. Matumizi ya teknolojia yatahamasishwa ili kuzalisha bidhaa bora zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya soko. Matokeo yanatarajiwa kuleta ongezeko la ajira na maisha bora zaidi kwa wananchi.
6.Kuimarisha Umoja na Mshikamano wa kitaifa kwa kuimarisha mawasiliano ya kisiasa, jamii na kiuchumi kwa watu wa pande mbili za Muungano.
HITIMISHO.
Dr. Kamani alitumia pia nafasi kuwaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi kupitia wawakilishi wao kumchagua kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.