ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 19, 2015

TIMU YA TANITA VETERAN YAIBUKA NA UBINGWA MICHUANO YA KOMBO LA KOKA CUP KIBAHA

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
 
TIMU ya soka ya Veterani imeweza kuibuka na ubingwa baada ya kuichapa timu ya Phat fam fc kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali wa michuano ya kombe la Koka Cup kwenye uwanja wa shule ya msingi Tanita Wilayani Kibaha.
 
 Mashindano hayo ambayo iliadaliwa na Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvester Koka kwa lengo la kuweza kukuza na kuinua vipaji kwa vijana  yalizishirikisha timu 15 kutoka kata ya Mkuza.
 
Katika mtanange huo ambao ulihudhuriwa na umati wa mashabiki na wadau wa soka  kutoka maeneo mbali mbali ulikuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na timu zote mbili kucheza kwa kukamiana katika kipindi chote cha dakika tisini za mchezo.
 
Wachezaji wa timu ya Tanita veterani ndio waliokuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za wapinzani wao baada ya kuandika bao kukao katika dakika ya 32 bao pekee lililowekwa kimiani na mshambuliji wao wa kutumainiwa Hamisi Mwinyikondo.
 
Kuingia kwa bao hilo kulionekana kuwachanganya wachezaji wa timu ya Phat fam na kujipanga upya na kuanza kuongeza kasi kwa kufanya mashabulizi ya kushitukiza lakini kutokana na safu ya ulizni ya wapinzani wao kuwa imara iliweza kufanya timu ya Tanita kwenda mapumziko ikiwa mbele ya bao 1-0.
 
Kipindi cha pili timu ya Phat fam waliweza kufanya mabadiliko ambayo yaliweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo kwani yaliweza kuzaaa matunda kwa kusawazisha bao lililopachikwa na mchezaji Said Kitambi.
 
Mshambuliaji Shaban Madaraka wa timu ya Tanita neterani aliweza  kuwainua mashabiki wake baada ya kuandika bado la pili ambalo liliweza kudumu hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa na kufanya mchezzo huo kumalizika kwa tanita kuibuka kuwa mabingwa kwa ushindi huo wa mabao 2-1 dhidi ya Phat fam.
 
Kwa ushindi huo timu ya Tanita iliweza kutawazwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo ya koka cup ngazi ya Kata ya mkuza na kuzwadiwa kiasi cha shilingi laki tatu pamoja na ngao, huku mshindi wa pili phat fam ilizawadiwa shilingi laki mbili na ngao,ambapo timu ya Tanita fc ikishika nafasi ya tatu na kujinyakulia shilingi laki moja na ngao.
 
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvester Koka ambaye  ndio aliyekuwa mgeni rasmi alisema kwamba lengo la kuandaa michuano hiyo ni kwa ajili ya kusaka vipaji vipya kwa vijana wa Kibaha ambao wataweza kuunda timu moja ambayo iyakuwa ikishiriki katika ligi mbali mbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.