NA ALBERT G. SENGO: MWANZA
KUELEKEA mchezo wa kesho timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, leo asubuhi imefanya mazoezi yake ya mwisho tayari kuikabili timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) mchezo utakao chezwa kesho saa 10:30 jioni katika dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.
Tiketi za mchezo tayari zimekwishaanza kuuzwa katika kituo cha Uwanja wa Nyamagana kwa bei ya Tsh. 5,000/= kwa mzunguko, Tsh. 12,000/= kwa jukwaa kuu na Tsh. 20,000/= viti maalum jukwaa maalum.
Tayari mashabiki toka sehemu mbalimbali nchini wameanza kumiminika kwa wingi mjini hapa hasa ikizingatiwa kuwa safari hii wachezaji wa kimataifa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamejumuishwa kwenye kikosi hicho hivyo kuwa kivutio kwa mashabiki Kanda ya ziwa wenye uadimu wa michezo ya Kimataifa.
Kutoka kushoto ni Afisa Habari wa TFF Baraka Kizuguto, Kocha msaidizi wa Stars Salum Mayanga, mchezaji wa Stars Erasto Nyoni na nahodha wa timu hiyo Narub Canavaro. |
Akiongea na waandishi wa Habari katika Hoteli Lakairo jijini Mwanza, Kocha Msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chake kiko katika hali nzuri na sasa kilichobaki nimchezo wenyewe wa kesho.
Mayanga amesema vijana wake wote 22 walioko kambini wako fiti na wamethibitishwa kiafya na daktari wa timu, wamefanya mazoezi ya siku tano katika dimba la CCM Kirumba wakiwa na ari na morali ya hali ya juu tayari kuusaka ushindi hiyo kesho.
Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa soka wa mkoa wa Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao muda wote wa mchezo.
Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali. |
Lakairo Hotel iliyopo Kirumba jijini Mwanza ambako Taifa Stars imeweka kambi. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.