Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars ) chini ya kocha wake Mart Nooj, inatarajiwa kuwasili kesho (Jumanne) jijini Mwanza kwaajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi utakaofanyika Jumapili ya tarehe 29/03, 2015 uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Jumla ya wachezaji 27 watatua Rock City majira ya saa 2:00 asubuhi ili kuizoea hali ya hewa ya jijini Mwanza sanjari na kusoma mazingira ambapo kwa sasa muda mwingi ni joto.
Kikosi cha Stars kinachotegemewa kutua hiyo kesho asubuhi ni; Magolikipa, Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Aggrey Morris (Azam FC), Mwinyi Haji (KMKM), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Oscar Joshua (Yanga), Abdi Banda na Hassan Isihaka (Simba SC).
Viungo ni Frank Domayo, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mcha Khamis (Azam FC), Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United), washambuliaji Mwinyi Kazimoto (Al Markhiry - Qatar),
Saimon Msuva , Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta (Tp Mazembe - Congo DR), John Bocco (Azam FC), na Juma Luizio (Zesco United - Zambia)
Timu ya Taifa ya Malawi inatarajiwa kuwasili jijini Mwanza machi 27, 2015 ikiwa na kikosi kamili, wakiwemo wachezaji nane wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, Msumbuji, Congo DR na Zimbambwe.
Malawi inashika nafasi ya 91 katika viwango vipya vya FIFA Duniani vilivyotolewa mwezi huu, huku Tanzania ikipanda kwa nafasi saba na kushika nafasi ya 100.
Tayari Shirikisho la soka la nchini Malawi limetuma majina ya wachezaji, benchi la ufundi na viongozi waandamizi watakao ambatana na timu hiyo.
FOOTBALL ASSOCIATION OF MALAWI
DELEGATION TO TANZANIA
1. Foreign based players
1. Joseph Kamwendo
2. Chimango Kaira
3. Frank Banda
4. Esau Kanyenda
5. Harry Nyirenda
6. Limbikani Mzava
7. Gerald Phiri
2. Local based player
1. McDonald Harawa
2. Richard Chipuwa
3. Lucky Malata
4. John Lanjesi
5. Francis Mulimbika
6. John Banda
7. Earnest Tambe
8. Micium Mhone
9. Chikoti Chirwa
10. Peter Wadabwa
11. Amos Khamula
Officials
1. Young Chimodzi - Head Coach
2. Jack Chamangwana - Assistant Coach
3. Franco Ndawa - Team Manager
4. Philip Nyasulu - Goalkeepers Trainer
5. Levison Mwale - Team Doctor
6. James Sangala - Teams' Liaison Officer
7. Alexander Waya - Head of Delegation (Executive Committee)
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.