Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraj Mtaturu (aliyevishwa sikafu), akipokea salamu kutoka kwa Chipukizi juzi baada ya kuwasili wilayani Ukerewe kwa ajili ya kuanza ziara ya siku tatu. |
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraj Mtaturu, akizungumza na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Ukerewe (hawapo pichani) wakati alipoanza ziara ya kikazi na kujitambulisha. |
NA PETER FABIAN,
WA GSENGO BLOG
NANSIO.
KATIBU mpya wa CCM mkoani Mwanza, Miraji Mtaturu, amewacharukia viongozi ‘mizigo’ na ameagiza viongozi kupitia vikao vya Chama kuwashughulikia haraka wana CCM waliokisaliti Chama na kupelekea kupoteza Jimbo la Ukerewe kwa kuwatosa na ikibidi kufukuzwa uanachama.
Mtaturu alitoa kauli hiyo leo kwa uongozi wa Chama hicho Wilayani Ukerewe, alisema, kosa kubwa na lisilosameheka katika Chama ni usaliti, adhabu yake ni kufukuzwa hivyo Chama kisibebe mizigo ya viongozi na wanachama wasaliti, kiitue kuliko kuendelea kukaa na nyoka ambapo ukifika wakati huwang’ata.
Mtaturu ambaye yupo katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwake wakati akizungumza na viongozi wa CCM, muda mfupi baada ya kuwasili mjini hapa.
“Maeneo yote nchini tulipopoteza majimbo, Kata, Mitaa, vijiji na Vitongoji katika uchaguzi zilizopita, CCM tuliponzwa na baadhi ya viongozi na wanachama wetu kutokana na mchango mkubwa wa kuwagawa kwa sababu ya kusigina katika demokrasia ndani ya Chama na kubeba wagombea wasiokubalika na kuuzika kwa wapiga kura,”alisisitiza
Katibu huyo alifafanua kuwa baadhi ya viongozi tumekuwa na utaratibu wa kuwaita wanachama na kuwambia wavunje makundi, lakini kumbe sisi waohao tumebeba watu ?,” Alihoji Katibu huyo na kudai ni ‘shida’ kuendelea kubeba mizigo ya viongozi na watu waliokigawa na kukisaliti Chama, tujipangeni kurejesha Jimbo la Ukerewe kwa kushirikiana wote.
Mtaturu alisema kuwa, watu wa aina hiyo wakiachwa wataendelea kuwemo ndani ya nyadhifa za Chama na kushiriki vikao wataendelea na tabia yao ya kukimaliza Chama hivyo huku kanuni zilizowekwa kuwashughulikia sasa zikitakiwa zitumike ili waende kwenye vyama walivyosaidia ili ijulikane wazi kuwa wao ni wapinzani wa CCM.
“Kosa kubwa CCM lisilosameheka ni kukisaliti Chama, adhabu yake ni kuondolewa katika Chama, viongozi tuamue mambo tusibebe mizigo, waliosaliti CCM na kusaidia wapinzani kushinda, timueni waeleweke kuwa ni maadui na tupambane nao nje, lakini ni vyema tukawa na mtililiko mzuri wa kuwafikia wananchi kwa utaratibu wa kuanzia mashina, matawi na kata,” alisisitiza.
Alikemea tabia ya viongozi hao kwamba, kuwa CCM siyo kuvaa kilemba sheti zuri la CCM lililo lenye maneno, ni kutekeleza kanuni, miiko na maadili pamoja na ahadi zake kwani nkubeba wagombea kwa sababu ya rushwa kunachangia baadhi ya wana chama wengine kuweka mikakati na kuiba fedha kwa ajili ya kampeni.
“Niwambie wananchi wengi bado wanaiamini na kuipenda CCM shida ni wao viongozi kukumbatia watu wenye pesa na kuacha watu wenye uwezo na kukubalika kwa wananchi wengi na kukifanya Chama wakati wa uchaguzi kuwa cha wenye pesa’
Katibu huyo aliyehamia mkoani Mwanza siku 18 zilizopita akitokea wilayani Iringa, awaliwaonya UVCCM na Jumuia ya Wazaizi ambayo alidai ipoipo bila mipango, pia waache udalali wa kubeba wagombea badala yake washirikiane kikamilifu na Chama kuengua viongozi na wagombea mizigo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.