ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 12, 2014

TOTO AFRICANS YAPORA DHAHABU ZA GEITA.


NA. ALBERT G. SENGO: MWANZA

KUPUUZA kanuni za soka, pamoja na kutozingatia sheria zake hii leo kumeigharimu timu ya Geita Gold na hatimaye kupokea kichapo kama cha mbwa mwizi vile toka kwa Toto Africans, bao 4-2 toka kwenye mchezo wa Ligi soka daraja la kwanza Tanzania Bara uliochezwa leo dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Tukio lililoacha wengi vinywa wazi ni lile la dakika ya 86 la mchezaji wa Geita Gold, Hussein Moshi, kumpiga refa, kumnyang'anya kadi na filimbi kisha kuvitupa mbali vitendea kazi hivyo, hilo likijitokeza mara baada ya mwamuzi wa mchezo huo Michael Magoli kutoka jijini Dar es salaam kumlima kadi ya njano golikipa wa Geita, Emmanuel Sangra kwa kudaka mpira nje ya eneo la 18, naye Hussein Moshi kumghasi mwamuzi huyo wa kati akimsukuma na kuzungumza naye kwa lugha zisizofaa kwa madai ya kuikandamiza Geita.

Mwamuzi alimlima Hussein Moshi kadi nyekundu ikiwa ni ya pili baada ya kadi ya awali ya njano aliyopata mchezaji huyo kama onyo.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa mkali na wenye undava na matukio mengi,  Geita ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza ikiwa ni katika sekunde ya 50 baada ya kipyenga cha kuanza mchezo kupulizwa mfungaji akiwa ni Kaisi Pastory.

Dakika 9 baadaye TOTO wanasawazisha kupitia Wilius Kimara.

Dakika ya 36 Geita wanaongeza bao la pili mfungaji akiwa ni yuleyule Kaisi Pastory.

Hadi mapumziko Geita wanaongoza 2-1 dhidi ya Toto.
Mashabiki wa Toto.
Kipindi cha pili dakika ya 53 Mwita Kemaronge anaipatia bao la 2 na la kusawazisha. Kisha anaongeza la 3 dakika ya 70.

Dakika ya 90 kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa kwa kipa wa Geita Emmanuel Sangra kudaka nje ya eneo lake la kujidai, Toto inapata bao la 4 na la ushindi mfungaji akiwa ni Mohamed Aziz.
Kocha John Tegete anazungumza mara baada ya mchezo.
 BOFYA PLAY KUSIKILIZA KAULI YA TEGETE.
Dakika 90 zinamalisika Toto 4-0 Geita.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.