NA PETER FABIAN, MWANZA.
KIDUMU na Bendi yake ya Bodaboda kutoka nchini Kenya
atamba kutoa burudani ya nguvu ili kusuuza mioyo ya mashabiki wa muziki dansi
wakati wa usiku wa vunja jungu ndani ya mpambano wa bendi tatu jijini Mwanza.
Akiongea nami kwa njia ya simu kutoka jijini
Nairobi nchini Kenya, Kidumu ambaye ni mwanamuziki anayemiliki bendi hiyo
alisema kwamba, mashabiki wa Jiji la Mwanza wasiwe na wasi kwakuwa lugha ya
Kiswahili haimpatii shida na atapiga nyimbo zake zikiwemo alizoimba kwa lugha
hiyo.
“Nakuja Jiji la Mwanza kutoa burudani na siyo kuuza
sura hivyo mashabiki wangu wataona na kushuhudia jinsi bendi yao ya bodaboda
ikifanya vitu adimu jukwaani na hakuna ubishi kazi itafanyika ili kuweka
heshima kwa mashabiki,”alisisitiza.
Aidha mwanamuziki huyo alieleza kuwa hana wasiwasi
na kupambanishwa na bendi yayote ya muziki katika nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwani anajiamini kwa kazi za kutoa burudani kwa mashabiki hivyo
naomba sapoti kutoka kwao ili kwani bila wao hakuna muziki jukwaani.
“Tumejipanga
na mashabiki watakaofika watapata ladha na vionjo tofauti kutokana na show
itakayofanywa na Bodaboda bendi, lakini natumai Malaika bendi na Super
Kamanyola nao wako vizuri na wamejipanga ili kuona nani zaidi kwenye mpambano
huo,”alisema mwanamuziki huo.
Kwa upande wake meneja wa burudani wa Villa Park
Resort Ramadhan Maganga alisema kwamba bendi ya hizo tatu za Bodaboda chini ya
kiongozi wake Kidumu kutoka nchini Kenya, wakati bendi ya Malaika itaambatana
na mkali wake Christian Bella toka jijini Dar es salaam na Super Kamanyola wenyeji
wa jijini watakuwa chini ya wakali wao Benovila Anthon, Roy Makuna na Rashidi Mwezingo.
Maganga amewataka mashabiki “wafike kujionea cheche za nani mkali zaidi wa bendi
na madj siku hiyo katika usiku wa vunja jungu ambao tumeandaa mambo makubwa
ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa huduma ya vyakula na vinywaji pamoja na
ulinzi wa hali ya juu kwa mali watakazokuja na kuziacha nje ikiwemo usalama wa
magari kwa asilimia 100 na hakuna vurugu,”alisisitiza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.