ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 27, 2014

MSHINDI WA REDD'S MISS SIMIYU KUJINYAKULIA KITITA CHA SH. MILIONI 6.5

Baadhi ya warembo kumi kati ya 16 watakaoshiriki shindano la REDD'S Miss Simiyu 2014/2015 wakiwa kambini Wilayani Busega mkoani Simiyu kujiandaa na shindano hilo linarotarajiwa kufanyika Juni 7 mwaka huu mkoani hapa. Picha Na Peter Fabian.
Mratibi wa shindano la REDD'S Miss Simiyu 2014 Omary Bakari (katikati) akiwa na Mkufunzi wa warembo Clara Ayoub kushoto kwake na baadhi ya warimbwende hao, baada ya mazoe kwenye kambi yao iliyopo katika hoteli ya Stop Over Wilayani Busega mkoani Simiyu. Picha Na Peter Fabian.

NA PETER FABIAN, MWANZA.
BUSEGA.                                           

MREMBO atakayeibuka mshindi wa shindano la Redds Miss Simiyu atajinyakulia kitita cha Sh. milioni 6.5 kutoka kwa mratibu wa shindano hilo Kampuni ya Respect Internment mratibu wa shindano hilo mkoani Simiyu.

Akingumza na gsengo blog Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Omary Bakari alisema kwamba, zawadi hiyo itatolewa kwa mrembo atakayeibuka mshindi wa kwanza (Miss) lakini pia wadhamini watakuwa na zawadi zingine ikiwemo kumpatia fursa ya kujiunga na chuo cha Musoma Utalii kilichopo mkoani Shinyanga kwa kozi atakayochagua mrimbwende aliyeshinda.

Bakari alieleza kuwa kutokana na shindano hilo kuwa la kwanza kufanyika katika Mkoa mpya wa Simiyu bado wanaangalia uwezekano wa kuongeza zawadi kwa washindi wa kwanza hadi wa tatu ili kureta hamasa zaidi kwa washiriki 16 waliopo kambini wakijifua kwa ajili ya shindano hilo.

"Warembo hawa 16 kutoka katika Wilaya zetu za Bariadi, Busega, Itilima, Maswa na Meatu waliopo kambini wote wanavigezo nani warembo hivyo tunatarajia mchuano utakuwa mkali na watu watashuhudia warembo wa kiwango cha kimataifa" alitamba.

Alifafanua kwamba, warembo hao 16 wako kambini katika hoteli ya Stop Over iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa lengo lakujifunza zaidi na kutambuoa moja ya rasilimali za taifa kwa kina na kufahamu wanyama waliopo kwenye hifadhi hiyo.

"Tunao warembo wenye vipaji hivyo watakaoshinda na kuchaguliwa kushiriki shindano la Kanda ya Ziwa wanaweza wakafanya vizuri zaidi na hatimae kwenda kushiriki fainali kitaifa ili kupata mrembo wa Redds Miss Tanzania 2014 akitokea Mkoa wa Simiyu,"alieleza.    


Mratibu wa shindano hilo, alisema kwamba katika kunogesha shindano hilo siku hiyo kwa mara ya kwanza wananchi wa Mkoa huo watashuhudia burudani kali kutoka kwa mwanzamuziki mashuhuri wa Muziki wa Taarabu nchini Mzee Yusufu na kundi zima la Jahazi Modern Taarab, Msanii wa Bongo Fleva H Baba na wasanii wengi kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wachekeshaji.

Bakari aliwataja wadhamini wa REDD'S Miss Simiyu 2014 kuwa ni  Kampuni ya Airtel, TBL kupitia kinywaji chake cha REDDs, Chuo cha Musoma Utalii Mkoa wa Shinyanga, Bhatt Electronic, Serengeti Stop Over, Benki ya CRDB, SBC kupitia kinywaji cha Peps, G&K Smart Hotel, Victoria Insitute, Matvila Beach na LP Gass Point.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.