MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)Umepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mkongwe wa muziki wa dansi nchini na aliyekuwa kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Muhidin Maalim Gurumo "Kamanda"aliyefariki Jumapili katika hospitali ya Muhimbili.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema jana kuwa wamepokea kwa majonzi makubwa na kusema kuwa pengo lake haliwezi kuzibika haraka kutokana na uwezo mkubwa aliokuwa nao wa kutunga, kuimba na kuongoza wanamuziki wenzake.
Alisema marehemu Gurumo hakuwa mtu wa kukata tamaa kuendeleza muziki wa dansi kwani aliwahi kuwafundisha wanamuzi wanaotamba katika bendi mbalimbali ikiwemo Msondo Ngoma..
"Kutoka miaka ya sitini Gurumo alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki akiwa na NUTA, JUWATA,Safari Sound,Sikinde na Msondo ambayo aliastaafu kabla ya kifo chake"alisema Taalib.
Wakati wa uhai wake, Gurumo alikuwa mwanachama wa SHIWATA na alikuwa kiunganishi cha wanamuziki wa Msondo Ngoma kushiriki kuunda kijiji cha wasanii Mkuranga mkoa wa Pwani na kubariki jitihada za kuwakomboa wasanii wa fani mbalimbali kujikomboa kiuchumi..
Marehemu Gurumo alitarajiwa kuzikwa jana Jumanne nyumbani kwao Masaki wilaya Kisarawe mkoa wa Pwani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.