Kilima cha Kanyama lilicho sababisha mauti, kilichokuwa kinamilikiwa na marehemu Mabina kwa kuridhiwa na serikali ya kijiji iliyotoa hati ya umiliki. |
Njia yenyewe ndiyo hii ambayo pia marehemu aliitumia kupita wakati akikimbia kujiokoa baada ya kundi la watu waliokuwa wakishambulia. |
Ni kona ambayo ndipo shambulizi lilianzia huku marehemu akijivuta taratibu kuelekea eneo la msaada. |
Marehemu alifika eneo hili akijaribu kukimbilia katika moja ya nyumba zinazo onekana mbele ili kupata msaada wa kujiokoa. |
Lakini kabla hajafika katika nyumba hizo eneo lililo zungushiwa duara ndipo alipo anguka baada ya kupigwa jiwe kichwani na kuanguka chini nakuanza kushambuliwa kwa mawe hadi mauti yalipomkuta. |
Kwa ukaribu zaidi na pembeni ni baadhi ya mawe yaliyo tumika kumshambulia. |
Ndivyo alivyokutwa na mauti mwenyekiti huyo wa zamani CCM. |
Nyumbani kwa marehemu na sehemu ya waombolezaji. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo (kulia) pamoja na Mkuu wa Usalama mkoa (kushoto) wakimfariji mjane wa marehemu Clement Mabina. |
Baadhi ya waombolezaji. |
Huzuni kubwa imetawala kwa wafanyakati wa Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) nyumbani kwa marehemu. |
Na. PETER FABIAN
WA G. SENGO BLOG.
WA G. SENGO BLOG.
WATU saba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya kinyama ya aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza na Diwani wa Kata ya Kisesa, Clement Mabina.
Watu hao wamekamatwa wakati hofu ikiwa imewakumba wakazi wa maeneo ya Kisesa na Kanyama, eneo ambalo marehemu Mabina aliuawa na watu wenye hasira katika kile kilichoelezwa kuwa mgogoro wa mashamba.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, SACP,Valentino Mulowola, akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu, alisema hadi sasa watu saba wanashikiliwa na jeshi hilo.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kwa nyakati tofauti jana,ambapo jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine wanaodaiwa kuhusika katika mauaji ya Mwenyekiti huyo wa zamani wa CM Mkoa wa Mwanza.
“Tunaendelea na upelelezi wa tukio hili la mauaji ya kinyama ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika na kuna maendeleo mazuri.Tuna washikilia watu saba wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji hayo,” SACP Mulowola
Katika tukio hilo la mauaji, Mabina aliuawa kwa kukatwa mapanga na kupigwa mawe ambapo alikutwa na majereha makubwa kichwani kichogoni.
Kabla ya kuawa na wananchi hao,marehemu alimpiga risasi mtoto Temeli Malemi kwa (11) bahati mbaya wakati akijihami na mashambulizi ya wananchi hao.
Ilielezwa jana na Kamanda wa Polisi SACP Mulowola kuwa marehemu alikutwa na silaha mbili aina ya Short-gun na bastola moja.
Hata hivyo ndugu wa marehemu walishindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari kuhusiana na habari zilizoandikwa na mitandao ya kijamii ikihusisha kifo cha Ndugu yao (Mabina) na masuala ya kisiasa.
Aidha habari kutoka eneo la tukio mmoja wa watuhumiwa waliokamatwa alikutwa na simu ya mkononi ya marehemu,hata hivyo kamanda hakutaka kutaja jina lake na watuhumiwa wengine kwa madai ya kuwa kutaja majina kungeweza kuvuruga upelelezi.
taarifa za baadhi ya watu waliokuwa wakinong’ono kuwa kundi linalosadikiwa kuhusika na mauaji hayo lilijiandaa kufanya kitendo hicho cha kinyama.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa tayari hofu kubwa na taharuki imewakumba wakazi wa kijiji cha Kanyama na baadhi wameyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa.
Kwa upande wa familia , mdogo wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Timoth Grigory Mabina alisema kwamba tangu kutokea kifo cha Kaka yake kumekuwa na upotoshwaji wa taarifa za tukio hilo unaofanywa na mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuripoti kwa utashi wa kisiasa zaidi kuliko ukweli.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu alisema kuwa taratibu za mazishi bado zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwasubili watoto wawili wa marehemu walioko nje ya nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alisema baada ya kupata taarifa za tukio hilo akiwa nje ya Mkoa huo alipokea kwa maskitiko makubwa na kushangazwa na watu ambao walitekeleza unyama huo baada ya kuamua kujichukulia sheria mkononi.
Mhandisi Ndikilo alisema kwamba serikali inaendelea kufanya uchunguzi wake kupitia vyuombo vya dola na kutoa wito kwa wananchi wa Kisesa na eneo la Kanyama kuwa watulivu na hakuna haja ya kukimbia nyumba zao kwa hofu ya kukamatwa na Polisi.
"Napenda kuwaeleza wananchi kuwa vyombo vya dola havitawakamata hovyo wananchi hao na wanaokimbia ni wale wanaodhaniwa ni waliotekeleza unyama na kutaka kuwa watulivu na kuisaidia serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuwakamata watu waliohusika na si vinginevyo.
Kwa mujibu wa taarifa za hivi punde baada ya kuwasili kwa kijana mkubwa wa marehemu kutoka nchini Uingereza zimeeleza kuwa huenda mazishi ya mwenyekiti huyo wa zamani wa CCM mkoa wa Mwanza, Mwenyekiti wa Halimashauri ya Wilaya ya Magu, Mjumbe wa Bodi ya NCU 1984 Ltd, Mjumbe wa Bodi ya MWAUWASA, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Mdau wa sekta ya Kilimo cha Pamba na mazao mengine ya chakula, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kisesa hadi mauti yanamkuta yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi juma hili.
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwasili kesho na kuhudhuria mazishi ya mama yake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Melick Sadiki aliyefariki leo sanjari na msiba huo wa mwenyekiti wa zamani ambaye alimuongoza kuomba kura kwa wananchi wa Mkoa huu katika Wilaya 7 katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 akiwa Mwenyekiti wa CCM kabla ya kushindwa uchaguzi wa CCM mwaka jana (2012) na mwenyekiti wa sasa Dkt. Anthony Dialo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.