Mkuu wa polisi wilaya ya Ilemela Debora Magiligimba akitoa nasaha kwa vijana 85 waliopata sifa ya kuwa polisi jamii tarafa ya Ilemela. |
Risala ya wahitimu wa mafunzo ya polisi jamii ilisomwa. |
Nao wahitimu wakaonyesha ukakamavu wakati wa kupambana na kujilinda na wahalifu. |
Parade. |
Kikazi zaidi. |
Hureeee...na vyeti vyao. |
Anaitwa Hamza Msafiri Katemi. |
MWANZA.
VIJANA
wa vikundi ya Polisi jamii Wilaya ya Ilemela wameonyesha ujasili na mafanikio
tangu kuanzishwa kwa Polisi Jamii kwenye Kata na kufanikiwa kukamata silaha
zilizotumika kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Kata na mitaa Wilayani
hapa.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kufunga mafunzo ya miezi mitatu ya Polisi Jamii kwa
kikundi cha vijana 85 waliomaliza kwenye uwanja wa Magomeni Kirumba Mkuu wa
Wilaya ya Ilemela Amina Masenza alisema kwamba kutokana na kuporomoka kwa misingi ya amani na
kuanza kujitokeza vitendo vingi vya uvunjifu wa amani na kuwepo matukio ya
uhalifu wa kutumia silaha Wilayani hapa.
Mkuu
huyo alisema kwamba kutokana na dunia sasa kukabiliwa na matishio mengi ya
kiusalama na vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha (wizi), uingizaji dawa za
kulevya , vitendo vya ujangiri na kuingia kwa wahamiaji haramu kumeanza
kuporomoka kwa misingi ya amani katika taifa letu jambo hili ni lazima lipigwe
vita kwa kila namna na kila mwananchi kwenye eneo lake.
“Tukubali
kutofautiana kwenye hoja zetu za kawaida na kisiasa lakini tukubaliane na
kushirikiana kudumiasha amani na umoja wetu na kuendeleza msingi iliyopo ya
kuwalinda wananchi na mali zao kwa kila mmoja kuwa askari huku kukiendela kuzingatia
matumizi ya sheria mkiwa wadau wakubwa wa ulinzi wa nchi kwenye maeneo
mbalimbali ya mitaa yetu tunakotoka” alisema
Mkuu
huyo wa Wilaya, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama
aliwataka wahitimu hao kuzingatia sheria na kufuata taratibu za kazi ya kulinda
maisha ya wananchi na mali zao kwa kushirikiana na Jeshi la polisi na viongozi
wa mitaa na Kata wanazotoka badala ya wao kuwa chanzo cha kuongezeka uhalifu
kutokana na kupata mafunzo na mbinu za kuwabaini na kuwakamata wahalifu.
“Siri ni
moja ya maadili ya mafunzo yetu lakini wajibu wenu pia ni kutoa taarifa kwa
viongozi wa mtaa, kata na vituo vya polisi wa Kata na Wilaya na kuhakikisha
mnashirikiana na jamii kwa kila mmoja, hii ndiyo dhana ya ulinzi shirikishi na
polisi jamii ambayo leo mmehitimisha mafunzo haya kwa muda wa miezi mitatu”
alisema.
Masenza
alisema mfumu huu wa ulinzi wa kushirikisha wananchi umelenga kumshirikisha
kila mmoja katika nafasi yake, kwa wakati wake na uwezo wake kubaini na kuzuia viashiria vya uhalifu na uhalifu
sehemu zao kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
“Ni
vyema mkatambua juhudi za serikali katika kuiweka nchi yetu katika hali ya
salama na amani, kupitia Jeshi la polisi nchini na vyombo vingine vya dola
pamoja na kuweka mikakati na kufanya operesheni mbalimbali lengo lake kubwa ni
kuifanya nchi kulindwa na raia na mali zao huku jeshi la polisi likitekeleza
mikakati na dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa vitendo ikiwemo utii
wa sheria bila shuruti.alisema na kuongeza
Kwamba
baada ya kuanzisha Polisi Kata, tukaazimia kuwa na Polisi jamii ya vikundi vya
vijana wenye mafunzo ya ukakamavu na mbinu ya kukamata wahalifu, jeshi la
polisi pia likaanzisha na kuweka Mkaguzi wa Polisi kila Tarafa huku pia kila
tarafa ikiwa na kikosi kazi kisichopungua askari 15kwa lengo la kusogeza,
kuimarisha na kutoa huduma za jeshi la polisi kwa wananchi.
Awali
Mkaguzi wa Polisi Tarafa ya Ilemela Joyce Kotecha aliyesimamia na kuhakikisha
vijana wanapatikana kushiriki mafunzo hayo kwa ihali alisema kwamba ilikuwa ni vigumu
kupata washiriki lakini baada ya kufanya vikao na wenyeviti na watendaji wa
mitaa na kuoa elimu kwa vijana, kisha
walionyesha nia na kukubali kushiriki mafunzo hayo ya Polisi Jamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.