Na Mwandishi Wetu,Kigoma
TIMU ya Makila Camp ya wanaume kutoka Manispaa ya Kigoma Ujiji imeshika nafasi ya kwanza katika mashindano mashindano ya Mitumbwi ya kupiga makasia na kujinyakulia kitita cha shilingi 900,000/- huku nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake ikienda kwa timu ya Mwamgongo Star walioibuka na kitita cha shilingi 700,000/-
Mashindano hayo ya kupiga Makasia mkoani hapa yamefanyika katika eneo la kibirizi katika Ziwa Tanganyika na kufadhiliwa na Kampuni ya bia nchini ya Tanzania Brewaries kupitia kinywaji chake cha Balimi ambacho ni maarufu sana kwa wakazi wa mikoa ya kanda ziwa.
Kwa upande wa wanaume zilishiriki timu 25 na upande wa wanawake timu 14 ziliingia kwenye kinyang’anyiro kila mtumbwi ukiwa na washiriki watano walioongoza kwa kupiga makasia na hatimaye kupata nafasi ya kuuwakilisha mkoa wa Kigoma kwenye mashindano ya kitaifa yatakayofanyika jijini Mwanza Desemba 7 mwaka huu.
Meneja mauzo wa TBL Kanda ya ziwa Sylivester Siza aalisema kuwa washindi hao waliopatikana wataowakilisha mkoa wa Kigoma katika mashindano ya kitaifa Mkoani mwanza.
Meneja huyo aliwataka washindi hao kutobweteka na ushindi huo badala yake aliwataka kutumia muda huu uliobaki kufanya mazoezi ya kutosha ili kuhakikisha wanaibuka washindi tena katika faini.
Rukia Haruna na Federina Ibrahim ni washiriki wakike katika mashindano hayo wamesema kuwa ule usemi wa wanawake wanaweza umetimia kwenye mashindano hayo mara baada ya kujitokeza kushiriki bila kinyongo licha ya kukabiliwa na changamoto za mfumo dume uliokuwa umewatenga kwa muda mrefu.
Waliwasihi wanawake wenzao wasiogope kujitokeza kwa wingi maeneo mengine mashindano hayao yanapoendelea kushiriki katika mashindano hayo kwa kudhani ni mchezo wa wanaume pekee kwani siku hzi haki ni sawa ni pamoja na michezo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.