Airtel yakabidhi vitabu vya milioni 10 sekondari 4 mkoa wa Dodoma
• Airtel yakabidhi vitabu kwa shule za sekondari Bihawane, Kibakwe, Itiso na Ndido mkoani Dodoma
Katika muendelezo wa kuhakikisha inatoa huduma zilizo bora kwa jamii nzima, Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu imefanikiwa kutoa vitabu vya kiada kwa shule mbalimbali zilizopo katika manispaa ya Dodoma.
Miongoni mwa shule zilizonufaika na mradi huo ni pamoja na Bihawane, Kibakwe, Itiso na Ndido zote zikiwa ni shule za sekondari katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alisema vitabu hivyo vitatumika kuendeleza elimu katika mkoa huo na kuwakwamua wengi katika utumwa wa kifikra.
“Udhamini huu wa Airtel utasaidia maendeleeo ya sekta ya elimu katika mkoa wetu wa Dodoma na kusaidia wanafunzi wengi waweze kuvutika katika usomaji wa vitabu mbalimbali kujikomboa na ujinga na umaskini ambao umekuwa ni tatizo kubwa sio tu kwa Dodoma bali kwa nchi nzima”.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Airtel kuchangia elimu nchini Meneja Mauzo wa Kanda Bw, Stephe Akyoo Alisema “Airtel inatoa vitabu hivi katika dhumuni la kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinainuka na kuleta ukombozi wa kiuchumi na kimaendeleo kwa jamii na nchi kiujumla”.
Nae Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bihawana Dodoma Crispin Mtesigwa alisema “Tunashukuru Airtel kwa kutoa vitabu hivi kwa shule mbalimbali za sekondari hapa nchini na huo ni mchango dhahiri wa maendeleo kwa nchi nzima. Ni jukumu letu sisi walimu na wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi vilivyotolewa na Airtel vinatumika kama ilivyokusudiwa”
Kupitia mradi huo wa shule yetu, mpaka sasa shule zaidi ya 1,000 zimeweza kunufaika na mradi huo kwa kujipatia vitabu vya kiada hasa kwenye masomo ya Fizikia, Hisabati, kemia na Biolojia. mradi huu wa Shule yetu unasambaza vitabu kwa shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na vitabu vya walimu kwa ajili ya kufundishia.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.