ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 27, 2013

WAZIRI WA USHIRIKIANO AFRIKA MASHARIKI ASHIRIKI IBADA YA HARAMBEE IGOMA JIJINI MWANZA


Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta, akitoa neno la shukurani kukaribishwa kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Katoliki Parokia ya igoma jijini Mwanza iliyofanyika tarehe 26 juni 2013.

Muonekano wa nje wa jengo la Kanisa la Katoliki Parokia ya igoma jijini Mwanza ambalo ujenzi wake unaendelea ambao hata hivyo hauwazuii waumini kufanya ibada.

Eneo la waumini waliohudhuria ibada hiyo ya harambee ya ujenzi kanisa katoliki parokia ya Igoma Mwanza.

Parokia ya Mt. Josephina Bakhita ina Vigango 6, Mitaa 11 yenye JNNK 117, Mapadri 3 wa shirika la Kanosa, masista 8 wa shirika la Bibi wa kilimanjaro, Makatekista 20 na waumini walei 6668 hivyo uimarishwaji wa ujenzi wa kanisa hili unapaswa kuharakishwa kukidhi mahitaji ya waumini.

Diwani wa Igoma mwenye elimu na mdogo kuliko wote, Mh. Adam Chagulani (mbele wa pili kutoka kulia akifurahia jambo ibadani).

Mpango wa ujenzi wa kanisa hili ulianza mwaka 2011 pale kanisa lilipobaini kuwa na ongezeko la waumini kutoka 700 hadi kufikia waumini 1300 ongezeko la asilimia 85, ambapo wengi waliishia kuadhimisha dominika nje ya kanisa.

Mnamo mwaka 2012 changizo la kwanza lilifanyika na kuweza kukusanya fedha na malighafi za ujenzi zilizokuwa na thamani ya zaidi ya Tshs 110,000,000/= zilizojenga msingi, kuta, kuezeka nusu jengo na kulipia gharama za mkandarasi kama linavyooneka.

Lengo la mualiko huu wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta ni kufanikisha harambee kwa kukusanya zaidi ya shilingi 150,000,000/=

Kwaya ikihudumu.

Lengo litakapotimia changamoto hii ya waumini kusali katika mazingira ya wazi na kusimama itatoweka, kwani Pamoja Tunaweza.

Kauli mbiu ya Ujenzi huu ni: "Ujenzi wa kanisa Igoma kwa Msaada wa Mungu na kwa nguvu zetu Wenyewe Tunaweza"

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta, akikagua maeneo ya jengo la kanisa mara baada ya ibada ya kuelekea Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Katoliki Parokia ya igoma jijini Mwanza iliyofanyika tarehe 26 juni 2013.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.