ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 1, 2013

LICHA YA JITIHADA ZA MBUNGE WA RORYA BADO KUNA CHANGAMOTO KUBWA KATIKA ELIMU JIMBONI KWAKE.

Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo (mwenye kofia mbele kushoto) akikagua majengo ya shule ya Kiradyenya iliyoko katika kitongozi cha Kiradyenya  ndani ya kijiji cha Ladyenya wilayani Rorya mkoani Mara kwa ajili ya kujionea hali halisi ya majengo kwa usalama wa wanafunzi wanaosoma shueni hapo pamoja na changamoto zinazo wakabili.


Shughuli za ukaguzi zikiendelea darasa moja hadi jingine.


Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo (mwenye kofia nyeupe) akionyeshwa mipaka ya shule na kingo mbalimbali kwenye ziara yake aliyoifanya kabla ya kuingia mwaka mpya wa 2013 wilayani Rorya mkoani Mara kwa ajili ya kujionea hali halisi ya majengo, ujenzi aliouanzisha kwenye shule mbalimbali pamoja na changamoto zinazo zikabili shule hizo.


Jiwe la msingi lashule hii limewekwa na ....


Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo (mwenye kofia mbele kushoto) akiingia kwenye moja ya madarasa ya shule ya Kiradyenya iliyoko katika kitongozi cha Kiradyenya  ndani ya kijiji cha Ladyenya wilayani Rorya mkoani Mara kujionea hali halisi...


Moja kati ya masuala yaliyoibuliwa na Mhe. Lameck Airo kama mapungufu kwa ujenzi wa shule hii ni ujenzi hafifu usio zingatia kanuni za usalama hasa katika suala la upauaji, hakuna lenta nazo kenchi za mabati zimeshikizwa kwenye matofali ya udongo bila cement, hali ambayo ni hatari kwani ni rahisi kwa mabati hayo kuezuliwa pindi mvua kubwa itakaponyesha au upepo makali ukivuma.    


Chunguza kwa umakini eneo la juu la darasa hili ni umaliziaji wa ubabaishaji. Ambapo mbunge Airo ameagiza kufanyika kwa marekebisho ya haraka kabla ya watoto kurejea kutoka kwenye likizo.


Mwenyekiti wa kata ya Kiradyenya Daudi Okong'o (aliyenyoosha mkono) akitoa maelezo kwa mbunge na msafara wake, juu ya kukwama kwa ujenzi wa moja ya madarasa yanayojengwa kwa nguvu za wananchi kokana na michango kutofikia malengo. 




Mbunge wa Rorya akiwa ameandamana na msafara wake akitoka kukagua nyumba ya mwalimu mkuu wa shule hiyo ambayo pia haijakamilika ujenzi wake, Mhe. Airo ameahidi kuchangia umaliziaji wa nyumba hiyo ya mwalimu mkuu.


Mbunge wa Rorya akiwa ameandamana na msafara wake akitoka kukagua nyumba za walimu wa shule hiyo zilizo hatua chache toka shuleni hapo ambazo kwazo zina hali ya kuridhisha, zikiwa na faida ya kuwarahisishia waalimu hao kuwahi kazini na kuwapunguzia gharama za huduma ya usafiri..


Hili ni goli na hiki ni kiwanja cha mpira wa pete aka netiboli shuleni hapa chenye mabonde ya hapa na pale, jeh kwa hali hii tutapata wachezaji mahiri au ni kuishia hapa hapa?


Nani kakwambia mganga hajigangi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.